Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mathayo 5

5
Sifa na heri
1 # Lk 6:20-49 Naye alipowaona makundi ya watu, alipanda mlimani; na alipokwisha kuketi, wanafunzi wake walimjia; 2akafumbua kinywa chake, akawafundisha, akisema,
3 # Isa 57:15 Heri walio maskini wa roho;
Maana ufalme wa mbinguni ni wao.
4 # Isa 61:2; Zab 126:5; Ufu 7:17 Heri wenye huzuni;
Maana hao watafarijika.
5 # Zab 37:11 Heri wenye upole;
Maana hao watairithi nchi.
6 # Isa 55:1-2 Heri wenye njaa na kiu ya haki;
Maana hao watashibishwa.
7 # Yak 2:13 Heri wenye rehema;
Maana hao watapata rehema.
8 # Zab 24:3-4; 51:10; 73:1; 1 Yoh 3:2,3 Heri wenye moyo safi;
Maana hao watamwona Mungu.
9 # Ebr 12:4 Heri wapatanishi;
Maana hao wataitwa wana wa Mungu.
10 # 1 Pet 3:14 Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki;
Maana ufalme wa mbinguni ni wao.
11 # 1 Pet 4:14 Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa ajili yangu. 12#2 Nya 36:16; Mdo 7:52; Yak 5:10; Ebr 11:33-38 Furahini, na kushangilia; kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni; kwa maana ndivyo walivyowaudhi manabii waliokuwa kabla yenu.
Chumvi na nuru
13 # Mk 9:50; Lk 14:34-35 Ninyi ni chumvi ya dunia; lakini chumvi ikipoteza ladha yake, ladha hiyo itarudishwa vipi? Haifai tena kabisa, ila kutupwa nje na kukanyagwa na watu.
14 # Yn 8:12; 9:5 Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji ukiwa juu ya mlima hauwezi kusitirika. 15#Mk 4:21; Lk 8:16; 11:33 Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani. 16#1 Pet 2:12; Efe 5:8,9 Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.
Sheria na Manabii
17 # Mt 3:15; Rum 3:31; 10:4 Msidhani ya kuwa nilikuja kuitangua Torati au Manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. 18#Lk 16:17; 21:33 Kwa maana, amin,#5:18 Amin: tazama 2 Kor 1:20 na Ufu 3:14. Maana yake ni Ni hakika, au Ni kweli hasa nisemayo. Hilo ni neno la Kiaramu lisilofasiriwa kwa Kigiriki. Ni neno lililotamkwa, kwa lugha iyo hiyo ya Kiaramu, na Yesu Kristo mwenyewe. Litumiwapo mwisho wa sala, maana yake ni Na iwe hivyo. nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie. 19#Yak 2:10; 1 Kor 15:9 Basi mtu yeyote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni. 20Maana nawaambia ya kwamba, Haki yenu isipozidi hiyo haki ya Waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.
Kuhusu hasira
21 # Kut 20:13; 21:12; Law 24:17; Kum 5:17; 17:8 Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiue, na mtu akiua, itampasa hukumu. 22#1 Yoh 3:15 Bali mimi nawaambieni, Kila amkasirikiaye ndugu yake itampasa hukumu; na mtu akimtusi ndugu yake, anastahili kuhukumiwa na baraza; na mtu akimwambia nduguye, Ewe mpumbavu, anastahili kuingia katika moto wa Jehanamu. 23#Mk 11:25 Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako, 24iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako. 25#Mt 6:14,15; 18:35; Lk 12:58,59 Patana na mshitaki wako upesi, wakati uwapo pamoja naye njiani; yule mshitaki asije akakupeleka kwa hakimu, na hakimu akakupeleka kwa askari, ukatupwa gerezani. 26Amin, nakuambia, Hutoki humo kamwe hadi utakapolipa senti ya mwisho.
Kuhusu uzinzi
27 # Kut 20:14; Kum 5:18 Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini; 28#Ayu 31:1; 2 Pet 2:14 lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake. 29#Mt 18:8,9; Mk 9:42,47; Kol 3:5 Jicho lako la kulia likikukosesha, ling'oe ulitupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee kuliko mwili wako wote utupwe katika Jehanamu. 30#Mt 18:8; Mk 9:43 Na mkono wako wa kulia ukikukosesha, ukate uutupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee kuliko mwili wako wote kutupwa katika Jehanamu.
Kuhusu talaka
31 # Kum 24:1-4; Mt 19:7; Mk 10:4 Imenenwa pia, Mtu akimwacha mkewe, na ampe hati ya talaka; 32#Mt 19:9; Mk 10:11-12; Lk 16:18; 1 Kor 7:10-11 lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa sababu ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini.
Kuhusu viapo
33 # Law 19:12; Hes 30:2; Kum 23:21; Kut 20:7 Tena mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiape uongo, ila mtimizie Bwana viapo vyako; 34#Yak 5:12; Isa 66:1; Mt 23:16-22; Mdo 7:49 lakini mimi nawaambia, Usiape kabisa; hata kwa mbingu, kwa maana ndicho kiti cha enzi cha Mungu; 35#Isa 66:1; Zab 48:2 wala kwa nchi, kwa maana ndipo pa kuwekea miguu yake; wala kwa Yerusalemu, kwa maana ndio mji wa Mfalme mkuu. 36Wala usiape kwa kichwa chako, maana huwezi kufanya unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi. 37#2 Kor 1:17; Yak 5:12 Bali maneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo; Siyo, siyo; kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu.
Kuhusu kujilipiza kisasi
38 # Kut 21:24; Law 24:20; Kum 19:21 Mmesikia kwamba imenenwa, Jicho kwa jicho, na jino kwa jino; 39#Lk 6:27-36 Lakini mimi nawaambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kulia, mgeuzie na la pili. #Yn 18:22,23; Law 19:18 40#1 Kor 6:7 Na mtu atakaye kukushitaki na kulichukua shati lako, mwachie na koti pia. 41Mtu yeyote akikulazimisha mwendo wa maili moja, nenda naye maili mbili. 42Akuombaye, mpe; naye atakaye kukopa kwako, usimpe kisogo.
Upendo kwa adui
43 # Law 19:18 Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako; 44#Kut 23:4,5; Rum 12:14,20; Lk 23:34; Mdo 7:59 lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi, 45#Efe 5:1 ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki. 46Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mnapata thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo? 47Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi sawa na hayo? 48#Law 19:2; Kum 18:13 Basi ninyi iweni wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.

Iliyochaguliwa sasa

Mathayo 5: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha