Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mathayo 4:2-4 - Compare All Versions

Mathayo 4:2-4 BHN (Biblia Habari Njema)

Akafunga siku arubaini mchana na usiku, na mwishowe akaona njaa. Basi, mshawishi akamjia, akamwambia, “Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, amuru mawe haya yawe mikate.” Yesu akamjibu, “Imeandikwa: ‘Mtu haishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno asemalo Mungu.’”

Shirikisha
Mathayo 4 BHN

Mathayo 4:2-4 SRUV (Swahili Revised Union Version)

Akafunga siku arubaini mchana na usiku, mwishowe akaona njaa. Mjaribu akamjia akamwambia, Ikiwa ndiwe Mwana wa Mungu, amuru mawe haya yawe mikate. Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.

Shirikisha
Mathayo 4 SRUV

Mathayo 4:2-4 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)

Akafunga siku arobaini mchana na usiku, mwisho akaona njaa. Mjaribu akamjia akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe haya yawe mikate. Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.

Shirikisha
Mathayo 4 SUV

Mathayo 4:2-4 NEN (Neno)

Baada ya kufunga siku arobaini usiku na mchana, hatimaye akaona njaa. Mjaribu akamjia na kumwambia, “Ikiwa wewe ndiwe Mwana wa Mungu, amuru mawe haya yawe mikate.” Lakini Yesu akajibu, “Imeandikwa: ‘Mtu haishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.’”

Shirikisha
Mathayo 4 NEN