Mathayo 3:1-4
Mathayo 3:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Siku zile Yohane Mbatizaji alitokea, akaanza kuhubiri katika jangwa la Yudea: “Tubuni, maana ufalme wa mbinguni umekaribia.” Huyu Yohane ndiye yule ambaye nabii Isaya alinena juu yake aliposema: “Sauti ya mtu anaita jangwani: ‘Mtayarishieni Bwana njia yake, nyosheni barabara zake.’” Yohane alivaa vazi lililoshonwa kwa manyoya ya ngamia, na ukanda wa ngozi kiunoni mwake. Chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwituni.
Mathayo 3:1-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Siku zile aliondokea Yohana Mbatizaji akihubiri katika nyika ya Yudea, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia. Kwa sababu huyo ndiye aliyenenwa na nabii Isaya, akisema, Sauti ya mtu aliaye nyikani, Itengenezeni njia ya Bwana, Yanyosheni mapito yake. Naye Yohana mwenyewe alikuwa na vazi lake la singa za ngamia, na mshipi wa ngozi kiunoni mwake; na chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwituni.
Mathayo 3:1-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Siku zile aliondokea Yohana Mbatizaji akihubiri katika nyika ya Uyahudi, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia. Kwa sababu huyo ndiye aliyenenwa na nabii Isaya, akisema, Sauti ya mtu aliaye nyikani, Itengenezeni njia ya Bwana, Yanyosheni mapito yake. Naye Yohana mwenyewe alikuwa na vazi lake la singa za ngamia, na mshipi wa ngozi kiunoni mwake; na chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwitu.
Mathayo 3:1-4 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Siku hizo Yohana Mbatizaji alikuja akihubiri katika nyika ya Yudea, akisema, “Tubuni, kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.” Huyu ndiye yule aliyenenwa habari zake na nabii Isaya aliposema: “Sauti ya mtu aliaye nyikani, ‘Itengenezeni njia kwa ajili ya Bwana, yanyoosheni mapito yake.’” Basi Yohana alivaa mavazi yaliyotengenezwa kwa singa za ngamia, akiwa na mkanda wa ngozi kiunoni mwake. Chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwitu.