Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mt 3

3
Mahubiri ya Yohana Mbatizaji
1 # Mk 1:1-8; Lk 3:3-18 # Lk 1:13 Siku zile aliondokea Yohana Mbatizaji akihubiri katika nyika ya Uyahudi, na kusema, 2#Mt 4:17; Mk 1:15Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia. 3#Isa 40:3; Yn 1:23Kwa sababu huyo ndiye aliyenenwa na nabii Isaya, akisema,
Sauti ya mtu aliaye nyikani,
Itengenezeni njia ya Bwana,
Yanyosheni mapito yake.
4 # 2 Fal 1:8 Naye Yohana mwenyewe alikuwa na vazi lake la singa za ngamia, na mshipi wa ngozi kiunoni mwake; na chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwitu.
5Ndipo walipomwendea Yerusalemu, na Uyahudi wote, na nchi zote za kandokando ya Yordani; 6naye akawabatiza katika mto wa Yordani, huku wakiziungama dhambi zao. 7#Mt 12:34; 23:33; Mwa 3:15Hata alipoona wengi miongoni mwa Mafarisayo na Masadukayo wakiujia ubatizo wake, aliwaambia, Enyi wazao wa nyoka, ni nani aliyewaonya ninyi kuikimbia hasira itakayokuja? 8Basi zaeni matunda yapasayo toba; 9#Yn 8:33,39; Rum 2:28,29; 4:12wala msiwaze mioyoni mwenu kwamba, Tunaye baba, ndiye Ibrahimu; kwa maana nawaambia ya kwamba Mungu aweza katika mawe haya kumwinulia Ibrahimu watoto. 10#Mt 7:19; Lk 13:6-9; Yn 15:6Na shoka limekwisha kuwekwa penye mashina ya miti; basi kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni. 11#Yn 1:15,26,27,33; Mdo 1:5Kweli mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba; bali yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu kuliko mimi, wala sistahili hata kuvichukua viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto. 12#Mt 13:30Ambaye pepeto lake li mkononi mwake, naye atausafisha sana uwanda wake; na kuikusanya ngano yake ghalani, bali makapi atayateketeza kwa moto usiozimika.
Kubatizwa kwa Yesu
13 # Mk 1:9-11; Lk 3:11-21; Yn 1:31-34 Wakati huo Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka Yordani kwa Yohana ili abatizwe. 14Lakini Yohana alitaka kumzuia, akisema, Mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu? 15Yesu akajibu akamwambia, Kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote. Basi akamkubali. 16Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake; 17#Mwa 22:2; Zab 2:7; Isa 42:1; Mt 12:18; 17:5; Mk 1:11; Lk 9:35na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.

Iliyochaguliwa sasa

Mt 3: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha