Mathayo 25:11-13 - Compare All Versions
Mathayo 25:11-13 BHN (Biblia Habari Njema)
Baadaye wale wasichana wengine wakaja, wakaita: ‘Bwana, Bwana, tufungulie!’ Lakini yeye akawajibu, ‘Nawaambieni kweli, siwajui nyinyi.’” Kisha Yesu akasema, “Kesheni basi, kwa maana hamjui siku wala saa.
Mathayo 25:11-13 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Halafu wakaja na wale wanawali wengine, wakasema, Bwana, Bwana, utufungulie. Akajibu akasema, Amin, nawaambia, siwajui ninyi. Basi kesheni, kwa sababu hamwijui siku wala saa.
Mathayo 25:11-13 SRUV (Swahili Revised Union Version)
Halafu wakaja na wale wanawali wengine, wakasema, Bwana, Bwana, utufungulie. Akajibu akasema, Amin, nawaambia, siwajui ninyi. Basi kesheni, kwa sababu hamwijui siku wala saa.
Mathayo 25:11-13 NEN (Neno)
“Baadaye wale wanawali wengine nao wakaja, wakaita, ‘Bwana! Bwana! Tufungulie mlango!’ “Lakini yeye bwana arusi akawajibu, ‘Amin, amin nawaambia, siwajui ninyi!’ “Kwa hiyo kesheni, kwa sababu hamjui siku wala saa.