Mathayo 2:19-20
Mathayo 2:19-20 Biblia Habari Njema (BHN)
Baada ya kifo cha Herode, malaika wa Bwana alimtokea Yosefu katika ndoto kule Misri, akamwambia, “Amka! Mchukue mtoto pamoja na mama yake, urudi tena katika nchi ya Israeli, maana wale waliotaka kumuua mtoto huyo wamekwisha kufa.”
Shirikisha
Soma Mathayo 2Mathayo 2:19-20 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Herode alipofariki, tazama, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto huko Misri, akasema, Inuka, umchukue mtoto na mamaye, ushike njia kwenda nchi ya Israeli; kwa maana wamekufa walioitafuta roho ya mtoto.
Shirikisha
Soma Mathayo 2Mathayo 2:19-20 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Hata alipofariki Herode, tazama, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto huko Misri, akasema, Ondoka, umchukue mtoto na mamaye, ushike njia kwenda nchi ya Israeli; kwa maana wamekufa walioitafuta roho ya mtoto.
Shirikisha
Soma Mathayo 2