Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mathayo 2

2
Wageni kutoka mashariki
1 # Lk 2:1-7 Yesu alipozaliwa katika Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme Herode, tazama, majusi wa mashariki walifika Yerusalemu, wakisema, 2#Hes 24:17 Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tuliiona nyota yake mashariki, nasi tumekuja kumsujudia. 3Basi mfalme Herode aliposikia hayo, alifadhaika, na Yerusalemu pia pamoja naye. 4Akakusanya wakuu wa makuhani wote na waandishi wa watu, akatafuta habari kwao, Kristo azaliwa wapi? 5#Mik 5:2; Yn 7:42 Nao wakamwambia, Katika Bethlehemu ya Yudea; kwa maana ndivyo ilivyoandikwa na nabii,
6 # Mik 5:1 Nawe Bethlehemu, katika nchi ya Yuda,
Hu mdogo kamwe miongoni mwa watawala wa Yuda;
Kwa kuwa kwako atatoka mtawala
Atakayewachunga watu wangu Israeli.
7Kisha Herode akawaita wale majusi faraghani, akapata kwao hakika ya muda tangu ilipoonekana ile nyota. 8Akawatuma Bethlehemu, akasema, Nendeni mkachunguze kwa makini habari za mtoto; na mkiisha kumwona, nileteeni habari, ili mimi nami niende nimsujudie. 9Nao waliposikia maneno ya mfalme, walishika njia; na tazama, ile nyota waliyoiona mashariki ikawatangulia, mpaka iliposimama juu ya mahali alipokuwapo mtoto. 10Nao walipoiona ile nyota, walifurahi furaha kubwa mno. 11#Zab 72:10,15; Isa 60:6 Wakaingia nyumbani, wakamwona mtoto pamoja na Mariamu mamaye, wakaanguka wakamsujudia; nao walipokwisha kufungua hazina zao, wakamtolea tunu; dhahabu, uvumba na manemane. 12Nao wakiisha kuonywa na Mungu katika ndoto wasimrudie Herode, wakaenda zao kwao kwa njia nyingine.
Yusufu akimbilia Misri
13 # Kut 2:15 Na hao walipokwisha kwenda zao, tazama, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto, akasema, Ondoka, umchukue mtoto na mama yake, ukimbilie Misri, ukae huko hadi nitakapokuambia; kwa maana Herode anataka kumtafuta mtoto amwangamize. 14Akaondoka akamchukua mtoto na mama yake usiku, akaenda zake Misri; 15#Hos 11:1 akakaa huko hadi Herode alipokufa; ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii, akisema,
Kutoka Misri nilimwita mwanangu.
Mauaji ya watoto wachanga
16Ndipo Herode, alipoona ya kuwa amedhihakiwa na wale majusi, alighadhibika sana, akatuma watu akawaua watoto wote wa kiume waliokuwako huko Bethlehemu na viungani mwake kote, kuanzia wenye miaka miwili na chini yake, kwa muda ule aliouhakikisha kwa wale majusi. 17#Yer 31:15 Ndipo lilipotimia neno lililonenwa na nabii Yeremia, akisema,
18 # Yer 31:15; Mwa 35:19 Sauti ilisikiwa Rama,
Kilio na maombolezo mengi,
Raheli akiwalilia watoto wake,
Asikubali kufarijiwa, kwa kuwa hawapo tena.
Yusufu arudi kutoka Misri
19Herode alipofariki, tazama, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto huko Misri, 20#Kut 4:19 akasema, Inuka, umchukue mtoto na mamaye, ushike njia kwenda nchi ya Israeli; kwa maana wamekufa walioitafuta roho ya mtoto. 21Akainuka akamchukua mtoto na mamaye, akaenda katika nchi ya Israeli. 22Lakini aliposikia ya kwamba Arkelao anatawala huko Yudea mahali pa Herode babaye, aliogopa kwenda huko; naye akiisha kuonywa katika ndoto, akaenda pande za Galilaya, 23#Mk 1:24; Lk 1:26; 2:39; Yn 1:45; Isa 11:1; 53:2 akaenda, akakaa katika mji ulioitwa Nazareti; ili litimie neno lililonenwa na manabii, Ataitwa Mnazareti.

Iliyochaguliwa sasa

Mathayo 2: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha