Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mathayo 13:44-45 - Compare All Versions

Mathayo 13:44-45 BHN (Biblia Habari Njema)

“Ufalme wa mbinguni unafanana na hazina iliyofichika shambani. Mtu mmoja aliigundua, akaificha tena. Alifurahi sana hata akaenda kuuza yote aliyokuwa nayo, akalinunua shamba lile. “Tena, ufalme wa mbinguni unafanana na mfanyabiashara mmoja mwenye kutafuta lulu nzuri.

Shirikisha
Mathayo 13 BHN

Mathayo 13:44-45 SRUV (Swahili Revised Union Version)

Tena ufalme wa mbinguni umefanana na hazina iliyositirika katika shamba; ambayo mtu alipoiona, aliificha; na kwa furaha yake akaenda akauza alivyo navyo vyote, akalinunua shamba lile. Tena ufalme wa mbinguni umefanana na mfanya biashara, mwenye kutafuta lulu nzuri

Shirikisha
Mathayo 13 SRUV

Mathayo 13:44-45 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)

Tena ufalme wa mbinguni umefanana na hazina iliyositirika katika shamba; ambayo mtu alipoiona, aliificha; na kwa furaha yake akaenda akauza alivyo navyo vyote, akalinunua shamba lile. Tena ufalme wa mbinguni umefanana na mfanya biashara, mwenye kutafuta lulu nzuri

Shirikisha
Mathayo 13 SUV

Mathayo 13:44-45 NEN (Neno)

“Ufalme wa mbinguni unafanana na hazina iliyofichwa shambani, ambayo mtu mmoja alipoiona akaificha tena. Kisha katika furaha yake, akaenda akauza vyote alivyokuwa navyo, akalinunua lile shamba. “Tena, ufalme wa mbinguni unafanana na mfanyabiashara aliyekuwa akitafuta lulu safi.

Shirikisha
Mathayo 13 NEN