Mathayo 10:6-8
Mathayo 10:6-8 Biblia Habari Njema (BHN)
Ila nendeni kwa watu wa Israeli waliopotea kama kondoo. Mnapokwenda hubirini hivi: ‘Ufalme wa mbinguni umekaribia.’ Ponyeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo. Mmepewa bure, toeni bure.
Mathayo 10:6-8 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Bali shikeni njia kuwaendea kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli. Na katika kuenda kwenu, hubirini, mkisema, Ufalme wa mbinguni umekaribia. Ponyeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure.
Mathayo 10:6-8 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Afadhali shikeni njia kuwaendea kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli. Na katika kuenenda kwenu, hubirini, mkisema, Ufalme wa mbinguni umekaribia. Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure.
Mathayo 10:6-8 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Lakini afadhali mshike njia kuwaendea kondoo wa nyumba ya Israeli waliopotea. Mnapoenda, hubirini ujumbe huu, ‘Ufalme wa mbinguni umekaribia.’ Ponyeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo wachafu. Mmepata bure, toeni bure.