Yona 3:1-3 - Compare All Versions
Yona 3:1-3 BHN (Biblia Habari Njema)
Neno la Mwenyezi-Mungu likamjia Yona mara ya pili: “Nenda Ninewi, ule mji mkuu, ukawatangazie watu ujumbe niliokupa.” Basi, Yona akaondoka, akaenda Ninewi kama Mwenyezi-Mungu alivyomwagiza. Mji wa Ninewi ulikuwa mkubwa sana. Upana wake ulikuwa mwendo wa siku tatu.
Yona 3:1-3 SRUV (Swahili Revised Union Version)
Neno la BWANA likamjia Yona mara ya pili, kusema, Ondoka, uende Ninawi, mji ule mkubwa; ukaihubiri habari nitakayokuamuru. Basi Yona akaondoka, akaenda Ninawi, kama Bwana alivyonena. Basi Ninawi ulikuwa mji mkubwa mno, ukubwa wake ni mwendo wa siku tatu.
Yona 3:1-3 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Neno la BWANA likamjia Yona mara ya pili, kusema, Ondoka, uende Ninawi, mji ule mkubwa; ukaihubiri habari nitakayokuamuru. Basi Yona akaondoka, akaenda Ninawi, kama Bwana alivyonena. Basi Ninawi ulikuwa mji mkubwa mno, ukubwa wake mwendo wa siku tatu.
Yona 3:1-3 NEN (Neno)
Ndipo neno la BWANA likamjia Yona mara ya pili: “Ondoka uende katika mji mkubwa wa Ninawi, ukautangazie ujumbe ninaokupa.” Yona akalitii neno la BWANA naye akaenda Ninawi. Basi Ninawi ulikuwa mji maarufu sana, ilichukua siku tatu kuuzunguka.