Yoeli 3:1-2
Yoeli 3:1-2 Biblia Habari Njema (BHN)
“Wakati huo na siku hizo nitakapoirekebisha hali ya Yuda na Yerusalemu, nitayakusanya mataifa yote, niyapeleke katika bonde liitwalo, ‘Mwenyezi-Mungu Ahukumu. Huko nitayahukumu mataifa hayo, kwa mambo yaliyowatendea watu wangu Israeli, hao walio mali yangu mimi mwenyewe. Maana waliwatawanya miongoni mwa mataifa, waligawa nchi yangu
Yoeli 3:1-2 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kwa maana, angalieni, siku zile, na wakati ule, nitakapowarudisha mateka wa Yuda na Yerusalemu, nitakusanya mataifa yote, nami nitawaleta chini katika bonde la Yehoshafati, na huko nitawahukumu kwa ajili ya watu wangu, na kwa ajili ya urithi wangu, Israeli, ambao wamewatawanya kati ya mataifa, na kuigawanya nchi yangu.
Yoeli 3:1-2 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kwa maana, angalieni, siku zile, na wakati ule, nitakapowarudisha mateka wa Yuda na Yerusalemu, nitakusanya mataifa yote, nami nitawaleta chini katika bonde la Yehoshafau, na huko nitawahukumu kwa ajili ya watu wangu, na kwa ajili ya urithi wangu, Israeli, ambao wamewatawanya kati ya mataifa, na kuigawanya nchi yangu.
Yoeli 3:1-2 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
“Katika siku hizo na wakati huo, nitakaporejesha neema ya Yuda na Yerusalemu, nitayakusanya mataifa yote na kuyaleta katika Bonde la Yehoshafati. Hapo nitaingia kwenye hukumu dhidi yao kuhusu urithi wangu, watu wangu Israeli, kwa kuwa waliwatawanya watu wangu miongoni mwa mataifa na kuigawa nchi yangu.