Yohane 7:49-51
Yohane 7:49-51 Biblia Habari Njema (BHN)
Lakini umati huu haujui sheria ya Mose; umelaaniwa!” Mmoja wao alikuwa Nikodemo ambaye hapo awali alikuwa amemwendea Yesu. Basi, yeye akawaambia, “Je, sheria yetu humhukumu mtu kabla ya kumsikia kwanza na kujua anafanya nini?”
Yohane 7:49-51 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Lakini makutano hawa wasioifahamu torati wamelaaniwa. Akawaambia Nikodemo, (naye ni yule aliyemwendea zamani, maana ni mmoja wao), Je! Torati yetu humhukumu mtu kabla ya kumsikia kwanza, na kujua atendavyo?
Yohane 7:49-51 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Lakini makutano hawa wasioifahamu torati wamelaaniwa. Akawaambia Nikodemo, (naye ni yule aliyemwendea zamani, maana ni mmoja wao), Je! Torati yetu humhukumu mtu kabla ya kumsikia kwanza, na kujua atendavyo?
Yohane 7:49-51 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Lakini umati huu wa watu wasiojua Sheria ya Musa, wamelaaniwa.” Ndipo Nikodemo, yule aliyekuwa amemwendea Yesu siku moja usiku, na alikuwa mmoja wao, akauliza, “Je, sheria zetu zinaturuhusu kumhukumu mtu kabla ya kumsikiliza na kufahamu alilotenda?”