Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yohana 7

7
Kutoamini kwa ndugu za Yesu
1 # Mk 9:30; Lk 9:51 Na baada ya hayo Yesu alikuwa akitembea katika Galilaya; maana hakutaka kutembea katika Yudea, kwa sababu Wayahudi walikuwa wakitaka kumwua. 2#Law 23:34; Kum 16:13 Na sikukuu ya Wayahudi, sikukuu ya vibanda, ilikuwa karibu. 3#Yn 2:12; Mt 12:46; Mdo 1:14 Basi ndugu zake wakamwambia, Ondoka hapa, uende Yudea, wanafunzi wako nao wapate kuzitazama kazi zako unazozifanya. 4Kwa maana hakuna mtu afanyaye mambo kwa siri, naye yeye mwenyewe anataka kujulikana. Ukifanya mambo haya, basi jidhihirishe kwa ulimwengu. 5#Mt 13:55 Maana hata nduguze hawakumwamini. 6#Yn 2:4 Basi Yesu akawaambia, Wakati wangu haujafika bado; ila wakati wenu sikuzote upo. 7#Yn 15:18 Ulimwengu hauwezi kuwachukia ninyi; bali hunichukia mimi, kwa sababu mimi naushuhudia ya kuwa kazi zake ni mbovu. 8Pandeni ninyi kwenda kula sikukuu; mimi sipandi bado kwenda kula sikukuu hii, kwa kuwa wakati wangu haujatimia. 9Naye alipokwisha kuwaambia hayo, alibaki huko Galilaya.
Yesu katika sikukuu ya vibanda
10Hata ndugu zake walipokwisha kupanda kuiendea sikukuu, ndipo yeye naye alipopanda, si kwa wazi bali kana kwamba kwa siri. 11Basi Wayahudi wakamtafuta kwenye sikukuu, wakasema, Yuko wapi yule? 12Kukawa na manung'uniko mengi katika makutano juu yake. Wengine wakasema, Ni mtu mwema. Na wengine wakasema, Sivyo; bali anawadanganya makutano. 13#Yn 9:22; 12:42; 19:38 Lakini hakuna mtu aliyemsema waziwazi, kwa sababu ya kuwaogopa Wayahudi.
14Hata ikawa katikati ya sikukuu Yesu alipanda kuingia hekaluni, akafundisha. 15#Mt 13:54; Lk 2:47 Wayahudi wakastaajabu wakisema, Amepataje huyu kujua elimu, ambaye hakusoma? 16#Yn 12:49 Basi Yesu akawajibu, akasema, Mafunzo yangu si yangu mimi, ila ni yake yeye aliyenituma. 17Mtu akipenda kuyatenda mapenzi yake, atajua habari ya yale mafunzo, kwamba yatoka kwa Mungu, au kwamba mimi nanena kwa nafsi yangu tu. 18#Yn 5:41,44 Yeye anenaye kwa nafsi yake tu hutafuta utukufu wake mwenyewe; bali yeye anayetafuta utukufu wake aliyemtuma, huyo ni wa kweli, wala ndani yake hamna udhalimu. 19#Yn 5:16,18,47; Mdo 7:53; Rum 2:17-29 Je! Musa hakuwapa torati? Wala hakuna mmoja wenu aitendaye torati. Mbona mnatafuta kuniua? 20#Mk 3:21; Yn 8:48,52; 10:20 Mkutano wakajibu, Ama! Una pepo! Ni nani anayetafuta kukuua? 21#Yn 5:16 Yesu akajibu, akawaambia, Mimi nilitenda kazi moja, nanyi nyote mnaistaajabia. 22#Mwa 17:10; Law 12:3 Musa aliwapa tohara; lakini si kwamba yatoka kwa Musa, bali kwa mababa; nanyi mwatahiri mtu siku ya sabato. 23#Yn 5:9 Basi ikiwa mtu hupashwa tohara siku ya sabato, ili Torati ya Musa isije ikavunjika, mbona mnanikasirikia mimi kwa sababu nilimfanya mtu kuwa mzima kabisa siku ya sabato? 24#Yn 8:15 Basi msihukumu kwa kuangalia kwa nje tu,#7:24 Katika Kigiriki ni ‘hukumu ya macho’. bali ifanyeni hukumu iliyo ya haki.
Huyu ndiye Kristo?
25 # Yn 7:19 Basi baadhi ya watu wa Yerusalemu wakasema, Je! Huyu siye wanayemtafuta ili wamwue? 26Na kumbe! Anena waziwazi, wala hawamwambii neno! Inawezekana hao wakuu wanajua hakika ya kuwa huyu ndiye Kristo? 27#Yn 7:41 Lakini huyu twamjua atokako; bali Kristo atakapokuja hakuna ajuaye atokako. 28Basi Yesu akapaza sauti yake hekaluni, akifundisha na kusema, Mimi mnanijua, na huko nitokako mnakujua; wala sikuja kwa nafsi yangu; ila yeye aliyenituma ni wa kweli, msiyemjua ninyi. 29#Mt 11:27 Mimi namjua, kwa kuwa nimetoka kwake, naye ndiye aliyenituma. 30#Yn 8:20; 13:1; Lk 22:53 Basi wakatafuta kumkamata; lakini hakuna mtu aliyeunyosha mkono wake ili kumshika, kwa sababu saa yake ilikuwa haijafika bado. 31#Yn 8:30; 10:42; 11:45; 12:42 Na watu wengi katika mkutano wakamwamini; wakasema, Atakapokuja Kristo, je! Atafanya ishara nyingi zaidi kuliko hizi alizozifanya huyu?
Maofisa watumwa kumkamata Yesu
32Mafarisayo wakawasikia mkutano wakinung'unika hivi juu yake; basi wakuu wa makuhani na Mafarisayo wakatuma watumishi ili wamkamate.
33 # Yn 13:33 Basi Yesu akasema, Bado kitambo kidogo nipo pamoja nanyi; kisha naenda zangu kwake yeye aliyenituma. 34#Yn 8:21; 13:36; 17:24 Mtanitafuta wala hamtaniona; nami nilipo ninyi hamwezi kuja. 35Basi Wayahudi wakasemezana, Huyu atakwenda wapi hata sisi tusimwone? Ati! Atakwenda kwa Utawanyiko wa Wagiriki, na kuwafundisha Wagiriki? 36Ni neno gani hilo alilolisema, Mtanitafuta wala hamtaniona; nami nilipo ninyi hamwezi kuja?
Mito ya maji yaliyo hai
37 # Law 23:36; Yn 4:10,14 Katika siku ya mwisho, siku ile kubwa ya sikukuu, Yesu akasimama, akapaza sauti yake akisema, Mtu akiona kiu, na aje kwangu anywe. 38#Eze 47:1,12; Zek 13:1; 14:8; Yoe 2:28; 3:18; Isa 44:3; 55:1; 58:11 Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake. 39#Yn 16:7; 2 Kor 3:17 Na neno hilo alilisema kuhusu Roho, ambaye wale wamwaminio watampokea baadaye; kwa maana Roho alikuwa hajaja, kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa.
Mgawanyiko kati ya watu
40 # Yn 6:14; Kum 18:15 Basi wengine katika mkutano walipoyasikia maneno hayo, walisema, Hakika huyu ndiye nabii yule. 41#Yn 1:46 Wengine walisema, Huyu ndiye Kristo. Wengine wakasema, Je! Kristo atoka Galilaya? 42#2 Sam 7:12; Mik 5:2; Mt 2:5,6; 22:42; Zab 89:3 Andiko halikusema ya kwamba Kristo atoka katika uzao wa Daudi, na kutoka Bethlehemu, mji ule alioukaa Daudi? 43#Yn 9:16 Basi kukaingia matengano katika mkutano kwa ajili yake. 44#Yn 7:30 Baadhi yao wakataka kumkamata, lakini hakuna mtu aliyenyosha mikono yake ili kumshika.
Kutoamini kwa wenye mamlaka
45 # Yn 7:32 Basi wale watumishi wakawaendea wakuu wa makuhani na Mafarisayo. Nao wakawaambia, Mbona hamkumleta? 46#Mt 7:28,29 Wale watumishi wakajibu. Hajanena kamwe mtu yeyote kama huyu anavyonena. 47Basi Mafarisayo wakawajibu, Je! Ninyi nanyi mmedanganyika? 48#Yn 12:42 Ni nani katika wakuu amwaminiye, au katika Mafarisayo? 49Lakini makutano hawa wasioifahamu torati wamelaaniwa. 50#Yn 3:1-2 Akawaambia Nikodemo, (naye ni yule aliyemwendea zamani, maana ni mmoja wao), 51#Kum 1:16,17; 19:15 Je! Torati yetu humhukumu mtu kabla ya kumsikia kwanza, na kujua atendavyo? 52#Yn 1:46; 7:41 Wakajibu, wakamwambia, Je! Wewe nawe umetoka Galilaya! Chunguza, na utaona kuwa Galilaya hakutatoka nabii.

Iliyochaguliwa sasa

Yohana 7: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha