Yohane 7:1-3
Yohane 7:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Baada ya hayo, Yesu alikuwa akitembea huko Galilaya. Hakutaka kutembea mkoani Yudea kwa sababu viongozi wa Wayahudi walikuwa wanataka kumuua. Sikukuu ya Wayahudi ya vibanda ilikuwa imekaribia. Basi, ndugu zake wakamwambia, “Ondoka hapa uende Yudea ili wanafunzi wako wazione kazi unazozifanya.
Yohane 7:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Na baada ya hayo Yesu alikuwa akitembea katika Galilaya; maana hakutaka kutembea katika Yudea, kwa sababu Wayahudi walikuwa wakitaka kumwua. Na sikukuu ya Wayahudi, sikukuu ya vibanda, ilikuwa karibu. Basi ndugu zake wakamwambia, Ondoka hapa, uende Yudea, wanafunzi wako nao wapate kuzitazama kazi zako unazozifanya.
Yohane 7:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Na baada ya hayo Yesu alikuwa akitembea katika Galilaya; maana hakutaka kutembea katika Uyahudi, kwa sababu Wayahudi walikuwa wakitafuta kumwua. Na sikukuu ya Wayahudi, Sikukuu ya Vibanda, ilikuwa karibu. Basi ndugu zake wakamwambia, Ondoka hapa, uende Uyahudi, wanafunzi wako nao wapate kuzitazama kazi zako unazozifanya.
Yohane 7:1-3 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Baada ya mambo haya, Yesu alienda sehemu mbalimbali za Galilaya. Hakutaka kwenda Yudea kwa sababu viongozi wa Wayahudi huko walitaka kumuua. Sikukuu ya Vibanda ya Wayahudi ilikuwa imekaribia. Hivyo ndugu zake Yesu wakamwambia, “Ondoka hapa uende Yudea ili wanafunzi Wako wapate kuona miujiza unayofanya.