Yakobo 4:4-7
Yakobo 4:4-7 Biblia Habari Njema (BHN)
Nyinyi ni watu msio na uaminifu kama wazinzi. Je, hamjui kwamba kuwa rafiki wa ulimwengu ni kuwa adui wa Mungu? Yeyote anayetaka kuwa rafiki wa ulimwengu anajifanya adui wa Mungu. Msifikiri kwamba Maandiko Matakatifu yamesema maneno ya bure, yanaposema: “Roho ambaye Mungu amemweka ndani yetu ana wivu mkubwa.” Lakini, neema tunayopewa na Mungu ina nguvu zaidi; kama yasemavyo Maandiko: “Mungu huwapinga wenye majivuno lakini huwapa neema wanyenyekevu.” Basi, jiwekeni chini ya Mungu; mpingeni Ibilisi naye atawakimbieni.
Yakobo 4:4-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu. Au mwadhani ya kwamba Maandiko yasema bure? Huyo Roho akaaye ndani yetu hututamani kiasi cha kuona wivu? Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu. Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.
Yakobo 4:4-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu. Au mwadhani ya kwamba maandiko yasema bure? Huyo Roho akaaye ndani yetu hututamani kiasi cha kuona wivu? Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu. Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.
Yakobo 4:4-7 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Ninyi wanaume na wanawake wazinzi, hamjui kwamba urafiki na dunia ni uadui na Mungu? Kwa hiyo mtu yeyote anayetaka kuwa rafiki wa dunia hufanyika adui wa Mungu. Au mwadhani kwamba Maandiko yasema bure kuwa huyo Roho ambaye Mungu amemweka ndani yetu hututamani kiasi cha kuona wivu? Lakini yeye hutupatia neema zaidi. Hii ndiyo sababu Maandiko yasema: “Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema.” Basi mtiini Mungu. Mpingeni ibilisi, naye atawakimbia.