Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yakobo 4

4
Urafiki na ulimwengu
1 # Rum 7:23; 1 Pet 2:11 Vita vyatoka wapi, na mapigano yaliyoko kati yenu yatoka wapi? Si humu, katika tamaa zenu zifanyazo vita katika viungo vyenu? 2Mwatamani, wala hamna kitu, mwaua na kuona wivu, wala hamwezi kupata. Mwafanya vita na kupigana, wala hamna kitu kwa kuwa hamwombi! 3Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu. 4#Lk 6:26; Rum 8:7; 1 Yoh 2:15 Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu. 5#Kut 20:3,5; Mt 6:24; Gal 5:17 Au mwadhani ya kwamba Maandiko yasema bure? Huyo Roho akaaye ndani yetu hututamani kiasi cha kuona wivu? 6#Mit 3:34; Ayu 22:29; Mt 23:12; 1 Pet 5:5 Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu. 7#Efe 6:12; 1 Pet 5:8,9 Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia. 8#Zek 1:3; Isa 1:16 Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili. 9Huzunikeni na kuomboleza na kulia. Kucheka kwenu na kugeuzwe kuwa kuomboleza, na furaha yenu kuwa huzuni kubwa. 10#1 Pet 5:6 Jidhilini mbele za Bwana, naye atawakuza.
Onyo juu ya kumhukumu mwingine
11Ndugu, msisingiziane; amsingiziaye ndugu yake, au kumhukumu ndugu yake, huisingizia sheria na kuihukumu sheria. Lakini ukiihukumu sheria, huwi mtenda sheria, bali umekuwa hakimu. 12#Mk 7:1; Rum 2:1; 14:4 Mtoa sheria na mwenye kuhukumu ni mmoja tu, ndiye awezaye kuokoa na kuangamiza. U nani wewe umhukumuye mtu mwingine?
Kujivuna juu ya kesho
13 # Mit 27:1 Haya basi, ninyi msemao, Leo au kesho tutaingia katika mji fulani na kukaa humo mwaka mzima, na kufanya biashara na kupata faida; 14#Lk 12:20; Zab 39:5,11 lakini hamjui yatakayokuwako kesho. Uzima wenu ni nini? Maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa muda mfupi tu, kisha hutoweka. 15#Mdo 18:21 Badala ya kusema, Bwana akipenda, tutakuwa hai na kufanya hivi au hivi. 16Lakini sasa mwajisifu katika majivuno yenu; kujisifu kote kwa namna hii ni kubaya. 17#Lk 12:47; Rum 14:23 Basi yeye ajuaye kutenda mema, wala hayatendi, kwake huyo ni dhambi.

Iliyochaguliwa sasa

Yakobo 4: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha