Yakobo 4:10-11
Yakobo 4:10-11 Biblia Habari Njema (BHN)
Nyenyekeeni mbele ya Bwana, naye atawainueni. Ndugu, msilaumiane nyinyi kwa nyinyi. Anayemlaumu ndugu yake na kumhukumu, huyo huilaumu na kuihukumu sheria. Kama ukiihukumu sheria, basi, wewe huitii sheria, bali waihukumu.
Yakobo 4:10-11 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Jidhilini mbele za Bwana, naye atawakuza. Ndugu, msisingiziane; amsingiziaye ndugu yake, au kumhukumu ndugu yake, huisingizia sheria na kuihukumu sheria. Lakini ukiihukumu sheria, huwi mtenda sheria, bali umekuwa hakimu.
Yakobo 4:10-11 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Jidhilini mbele za Bwana, naye atawakuza. Ndugu, msisingiziane; amsingiziaye ndugu yake, au kumhukumu ndugu yake, huisingizia sheria na kuihukumu sheria. Lakini ukiihukumu sheria, huwi mtenda sheria, bali umekuwa hakimu.
Yakobo 4:10-11 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Jinyenyekezeni mbele za Bwana, naye atawainua. Ndugu, msineneane mabaya ninyi kwa ninyi. Mtu yeyote anayesema mabaya dhidi ya ndugu yake au kumhukumu, anasema dhidi ya sheria na kuihukumu. Unapoihukumu sheria, basi huishiki sheria, bali umekuwa hakimu wa kuihukumu hiyo sheria.