Isaya 56:5-6
Isaya 56:5-6 Biblia Habari Njema (BHN)
nitampa nafasi maalumu na ya sifa katika nyumba yangu na kuta zake; nafasi bora kuliko kuwa na watoto wa kiume na wa kike: Nitampa jina la kukumbukwa daima, na ambalo halitafutwa kamwe. “Watu wageni watakaonikiri mimi Mwenyezi-Mungu, watakaoniheshimu, wakapenda jina langu na kuwa watumishi wangu, wote watakaoshika Sabato bila kuikufuru, watu watakaozingatia agano langu
Isaya 56:5-6 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nitawapa hawa nyumbani mwangu, na ndani ya kuta zangu, kumbukumbu na jina, lililo jema kuliko kuwa na watoto wa kiume na wa kike; nitawapa jina lidumulo milele, lisilokatiliwa mbali. Na wageni, walioandamana na BWANA ili wamhudumu, na kulipenda jina la BWANA, kuwa watumishi wake; kila aishikaye sabato asiivunje, na kulishika sana agano langu
Isaya 56:5-6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nitawapa hawa nyumbani mwangu, na ndani ya kuta zangu, kumbukumbu na jina, lililo jema kuliko kuwa na wana na binti; nitawapa jina lidumulo milele, lisilokatiliwa mbali. Na wageni, walioandamana na BWANA ili wamhudumu, na kulipenda jina la BWANA, kuwa watumishi wake; kila aishikaye sabato asiivunje, na kulishika sana agano langu
Isaya 56:5-6 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
hao nitawapa ndani ya Hekalu langu na kuta zake kumbukumbu na jina bora kuliko kuwa na watoto wa kiume na wa kike: nitawapa jina lidumulo milele, ambalo halitakatiliwa mbali. Wageni wanaoambatana na BWANA ili kumtumikia, kulipenda jina la BWANA, na kumwabudu yeye, wote washikao Sabato bila kuinajisi na ambao hushika sana agano langu