Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Isaya 56

56
Agano kuwafikia watiifu wote
1 # Mt 3:2; Rum 13:11 BWANA asema hivi, Shikeni hukumu, mkatende haki; kwa maana wokovu wangu uko karibu kuja, na haki yangu kufunuliwa. 2#Kut 20:11; Isa 58:13 Heri afanyaye haya, na mwanadamu ayashikaye sana; azishikaye sabato asizivunje, auzuiaye mkono wake usifanye uovu wowote. 3#Kum 23:1; Mdo 8:27; 1 Pet 1:1 Wala mgeni, aambatanaye na BWANA, asiseme hivi, Hakika yake BWANA atanitenga na watu wake; wala towashi asiseme, Mimi ni mti mkavu. 4Kwa maana BWANA awaambia hivi matowashi, wanaozishika sabato zangu, na kuyachagua mambo yanipendezayo, na kulishika sana agano langu; 5#Efe 2:22; 1 Tim 3:15; Ebr 3:6; Yn 1:12; Ufu 3:12 Nitawapa hawa nyumbani mwangu, na ndani ya kuta zangu, kumbukumbu na jina, lililo jema kuliko kuwa na watoto wa kiume na wa kike; nitawapa jina lidumulo milele, lisilokatiliwa mbali. 6Na wageni, walioandamana na BWANA ili wamhudumu, na kulipenda jina la BWANA, kuwa watumishi wake; kila aishikaye sabato asiivunje, na kulishika sana agano langu; 7#1 Pet 1:1; 2:5; Zab 4:5; Mal 1:11; Rum 12:1; Ebr 13:15; Mt 21:13; Mk 11:17; Lk 19:46 Nitawaleta hao nao hadi katika mlima wangu mtakatifu, na kuwafurahisha katika nyumba yangu ya sala; makafara yao na dhabihu zao zitakubaliwa juu ya madhabahu zangu; kwa maana nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote. 8#Mwa 49:10; Isa 43:6; Efe 1:10 Bwana MUNGU, akusanyaye waliofukuzwa katika Israeli asema, Pamoja na hayo nitamkusanyia na wengine, zaidi ya hao walio wake waliokusanywa.
Ufisadi wa watawala wa Israeli
9Enyi wanyama wote wa porini njoni
Mle, enyi wanyama wote wa porini.
10 # Mt 15:14; Flp 3:2 Walinzi wake ni vipofu, wote pia hawana maarifa; wote ni mbwa walio bubu, hawawezi kulia; huota ndoto, hulala, hupenda usingizi. 11Naam, mbwa hao wana uchu sana, hawashibi kamwe; na hao ni wachungaji wasioweza kufahamu neno; wote pia wamegeuka upande, wazifuate njia zao wenyewe, kila mmoja kwa faida yake, toka pande zote. 12Husema,
Njooni, nitaleta divai,
Na tunywe sana kileo;
Na kesho itakuwa kama leo,
Sikukuu kupita kiasi.

Iliyochaguliwa sasa

Isaya 56: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha