Isaya 29:8
Isaya 29:8 Biblia Habari Njema (BHN)
Mataifa yote yanayoushambulia mji wa Yerusalemu yatakuwa kama mtu mwenye njaa anayeota anakula lakini aamkapo bado anaumwa na njaa! Au mtu mwenye kiu anayeota kuwa anakunywa, lakini anaamka mdhaifu, bado ana kiu.
Isaya 29:8 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Tena itakuwa kama mtu mwenye njaa aotapo, kumbe, anakula; lakini aamkapo, nafsi yake haina kitu; na kama mtu mwenye kiu aotapo, kumbe, anakunywa; lakini aamkapo, kumbe, anazimia, na nafsi yake inatamani; hivyo ndivyo utakavyokuwa huo wingi wa mataifa waletao vita juu ya mlima Sayuni.
Isaya 29:8 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Tena itakuwa kama mtu mwenye njaa aotapo, kumbe, anakula; lakini aamkapo, nafsi yake haina kitu; na kama mtu mwenye kiu aotapo, kumbe, anakunywa; lakini aamkapo, kumbe, anazimia, na nafsi yake inatamani; hivyo ndivyo utakavyokuwa huo wingi wa mataifa waletao vita juu ya mlima Sayuni.
Isaya 29:8 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
kama vile mtu aliye na njaa aotavyo kuwa anakula, lakini huamka, bado njaa yake ingalipo, kama vile mtu mwenye kiu aotavyo kuwa anakunywa maji, lakini huamka akiwa anazimia, akiwa bado angali ana kiu. Hivyo ndivyo itakavyokuwa kwa makundi yote ya mataifa yanayopigana dhidi ya Mlima Sayuni.