Isaya 29:13-16
Isaya 29:13-16 Biblia Habari Njema (BHN)
Bwana asema, “Watu hawa huja kuniabudu kwa maneno matupu, hali mioyo yao iko mbali nami. Wananiheshimu kulingana na mapokeo ya watu tu, jambo walilojifunza wao wenyewe. Hivyo, nitawatenda tena watu hawa maajabu, mambo ya ajabu na ya kushangaza. Nao wenye hekima wao wataishiwa hekima, na busara ya wenye busara wao itatoweka. “Ole mnaomficha Mwenyezi-Mungu mipango yenu, mnaotenda matendo yenu gizani na kusema: ‘Hamna atakayetuona; nani awezaye kujua tunachofanya?’ Nyinyi mnafanya mambo kinyume kabisa! Je, mfinyanzi na udongo ni hali moja? Chombo hakiwezi kumwambia aliyekitengeneza: ‘Wewe hukunitengeneza.’ Kilichofinyangwa hakiwezi kumwambia aliyekiumba, ‘Wewe hujui chochote.’”
Isaya 29:13-16 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Bwana akanena, Kwa kuwa watu hawa hunikaribia na kuniheshimu kwa vinywa vyao, bali mioyo yao wamefarakana nami, na kicho chao walichonacho kwangu ni maagizo ya wanadamu waliyofundishwa; kwa sababu hiyo mimi nitafanya tena kazi ya ajabu kati ya watu hawa, kazi ya ajabu na mwujiza; na akili za watu wao wenye akili zitapotea, na ufahamu wa wenye busara wao utafichwa. Ole wao wanaojitahidi kumficha BWANA mashauri yao, na matendo yao yamo gizani, nao husema, Ni nani atuonaye? Nani atujuaye? Ninyi mnapindua mambo; Je! Mfinyanzi ahesabiwe kuwa kama udongo; kitu kilichofinyangwa kimnene yeye aliyekifinyanga, Hakunifinyanga huyu; au kitu kilichoumbwa kimnene yeye aliyekiumba, Yeye hana ufahamu?
Isaya 29:13-16 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Bwana akanena, Kwa kuwa watu hawa hunikaribia na kuniheshimu kwa vinywa vyao, bali mioyo yao wamefarakana nami, na kicho chao walicho nacho kwangu ni maagizo ya wanadamu waliyofundishwa; kwa sababu hiyo mimi nitafanya tena kazi ya ajabu kati ya watu hawa, kazi ya ajabu na mwujiza; na akili za watu wao wenye akili zitapotea, na ufahamu wa wenye busara wao utafichwa. Ole wao wanaojitahidi kumficha BWANA mashauri yao, na matendo yao yamo gizani, nao husema, Ni nani atuonaye? Nani atujuaye? Ninyi mnapindua mambo; Je! Mfinyanzi ahesabiwe kuwa kama udongo; kitu kilichofinyangwa kimnene yeye aliyekifinyanga, Hakunifinyanga huyu; au kitu kilichoumbwa kimnene yeye aliyekiumba, Yeye hana ufahamu?
Isaya 29:13-16 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Bwana asema: “Watu hawa hunikaribia kwa vinywa vyao na kuniheshimu kwa midomo yao, lakini mioyo yao iko mbali nami. Ibada yao kwangu inatokana na maagizo waliyofundishwa na wanadamu. Kwa hiyo mara nyingine tena nitawashangaza watu hawa, kwa ajabu juu ya ajabu. Hekima ya wenye hekima itapotea, nayo akili ya wenye akili itatoweka.” Ole kwa wale wanaoenda kwenye vilindi virefu kumficha BWANA mipango yao, wafanyao kazi zao gizani na kufikiri, “Ni nani anayetuona? Ni nani atakayejua?” Mnapindua mambo juu chini, kana kwamba mfinyanzi aweza kufikiriwa kuwa kama udongo wa mfinyanzi! Je, kile kilichofinyangwa chaweza kumwambia yule aliyekifinyanga, “Wewe hukunifinyanga mimi”? Je, chungu kinaweza kumwambia mfinyanzi, “Wewe hujui chochote”?