Isaya 25:7-9
Isaya 25:7-9 Biblia Habari Njema (BHN)
Katika mlima huuhuu, Mwenyezi-Mungu ataliondoa wingu la huzuni lililowafunika watu wote, kifuniko cha uchungu juu ya mataifa yote. Bwana Mungu atakiangamiza kifo milele! Atayafuta machozi katika nyuso za watu wote na kuwaondolea watu wake aibu duniani kote. Bwana Mwenyezi-Mungu ametamka. Siku ile, watu wote watasema, “Huyu ndiye Mungu wetu! Tumemngojea atuokoe. Huyu ndiye Mwenyezi-Mungu tuliyemtazamia. Njoni tufurahi na kushangilia kwa kuwa ametuokoa.”
Isaya 25:7-9 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Naye katika mlima huu atauharibu utando uliowekwa juu ya watu wote, na utaji ule uliotandwa juu ya mataifa yote. Amemeza mauti hata milele; na Bwana MUNGU atafuta machozi katika nyuso zote; na aibu ya watu wake ataiondoa katika ulimwengu wote; maana BWANA amenena hayo. Katika siku hiyo watasema, Tazama, huyu ndiye Mungu wetu, Ndiye tuliyemngoja atusaidie; Huyu ndiye BWANA tuliyemngoja, Na tushangilie na kuufurahia wokovu wake.
Isaya 25:7-9 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Naye katika mlima huu atauharibu uso wa sitara iliyowekwa juu ya watu wote, na utaji ule uliotandwa juu ya mataifa yote. Amemeza mauti hata milele; na Bwana MUNGU atafuta machozi katika nyuso zote; na aibu ya watu wake ataiondoa katika ulimwengu wote; maana BWANA amenena hayo. Katika siku hiyo watasema, Tazama, huyu ndiye Mungu wetu, Ndiye tuliyemngoja atusaidie; Huyu ndiye BWANA tuliyemngoja, Na tushangilie na kuufurahia wokovu wake.
Isaya 25:7-9 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Juu ya mlima huu ataharibu sitara ihifadhiyo mataifa yote, kile kifuniko kifunikacho mataifa yote, yeye atameza mauti milele. BWANA Mwenyezi atafuta machozi katika nyuso zote; ataondoa aibu ya watu wake duniani kote. BWANA amesema hili. Katika siku ile watasema, “Hakika huyu ndiye Mungu wetu; tulimtumaini, naye akatuokoa. Huyu ndiye BWANA, tuliyemtumaini; sisi tushangilie na kufurahia katika wokovu wake.”