aweka tena siku fulani, akisema katika Daudi baada ya muda mwingi namna hii, Leo, kama ilivyonenwa tangu zamani,
Leo, kama mkisikia sauti yake,
Msifanye mioyo yenu migumu.
Maana kama Yoshua angaliwapa pumziko, asingaliinena siku nyingine baadaye. Basi, limesalia pumziko la sabato kwa watu wa Mungu. Kwa maana yeye aliyeingia katika pumziko lake amepumzika mwenyewe katika kazi yake, kama vile Mungu alivyopumzika katika kazi zake.