Wagalatia 3:5-7
Wagalatia 3:5-7 Biblia Habari Njema (BHN)
Je, Mungu huwajalia Roho na kutenda miujiza kati yenu ati kwa sababu mnatimiza yanayotakiwa na sheria, ama kwa sababu mnasikia Injili na kuiamini? Chukueni kwa mfano habari za Abrahamu: Yeye alimwamini Mungu, naye Mungu akamkubali kuwa mwadilifu. Sasa basi, jueni kwamba watu wenye kumwamini ndio walio watoto halisi wa Abrahamu.
Wagalatia 3:5-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Basi, yeye awapaye Roho na kufanya miujiza kati yenu, je! Afanya hayo kwa matendo ya sheria, au kwa kusikia kunakotokana na imani? Kama vile Abrahamu alivyomwamini Mungu akahesabiwa haki. Fahamuni basi, ya kuwa wale walio wa imani, hao ndio wana wa Abrahamu.
Wagalatia 3:5-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Basi, yeye awapaye Roho na kufanya miujiza kati yenu, je! Afanya hayo kwa matendo ya sheria, au kwa kusikia kunakotokana na imani? Kama vile Ibrahimu alivyomwamini Mungu akahesabiwa haki. Fahamuni basi, ya kuwa wale walio wa imani, hao ndio wana wa Ibrahimu.
Wagalatia 3:5-7 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Je, Mungu huwapa Roho wake na kufanya miujiza kati yenu kwa sababu mnatii sheria, au kwa sababu mnaamini kile mlichosikia? Kama vile “Abrahamu alimwamini Mungu na ikahesabiwa kwake kuwa haki.” Fahamuni basi kwamba wale walio na imani, hao ndio watoto wa Abrahamu.