Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Wagalatia 3

3
Sheria au imani
1Enyi Wagalatia msio na akili, ni nani aliyewaloga, ninyi ambao Yesu Kristo aliwekwa wazi mbele ya macho yenu ya kuwa amesulubiwa? 2Nataka kujifunza neno hili moja kwenu. Je! Mlipokea Roho kwa matendo ya sheria, au kwa kusikia kunakotokana na imani? 3Je! Mmekuwa wajinga namna hii? Baada ya kuanza katika Roho, mnataka kukamilishwa sasa katika mwili? 4Mmepatikana na mateso makubwa namna hii bure? Ikiwa ni bure kweli. 5Basi, yeye awapaye Roho na kufanya miujiza kati yenu, je! Afanya hayo kwa matendo ya sheria, au kwa kusikia kunakotokana na imani? 6#Mwa 15:6; Rum 4:3 Kama vile Abrahamu alivyomwamini Mungu akahesabiwa haki.
7 # Rum 4:16 Fahamuni basi, ya kuwa wale walio wa imani, hao ndio wana wa Abrahamu. 8#Mwa 12:3; 18:18; Mdo 3:25 Na andiko, kwa vile lilivyoona tangu zamani kwamba Mungu atawahesabia haki Mataifa kwa imani, lilimhubiria Abrahamu Habari Njema zamani, kusema, Katika wewe Mataifa yote watabarikiwa. 9#Rum 4:16 Basi hao walio wa imani hubarikiwa pamoja na Abrahamu aliyekuwa mwenye imani. 10#Kum 27:26 Kwa maana wale wote walio wa matendo ya sheria, wako chini ya laana; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu asiyedumu katika yote yaliyoandikwa katika kitabu cha Torati, ayafanye. 11#Hab 2:4; Rum 1:17; Ebr 10:38 Ni dhahiri ya kwamba hakuna mtu ahesabiwaye haki mbele za Mungu katika sheria; kwa sababu Mwenye haki ataishi kwa imani. 12#Law 18:5; Rum 10:5 Na torati haikuja kwa imani, bali, Ayatendaye hayo ataishi katika hayo. 13#Kum 21:23; Rum 8:3; 2 Kor 5:21 Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti; 14ili kwamba baraka ya Abrahamu iwafikie Mataifa katika Yesu Kristo, tupate kupokea ahadi ya Roho kwa njia ya imani.
Ahadi kwa Abrahamu
15Ndugu zangu, nanena kwa jinsi ya kibinadamu. Lijapokuwa ni agano la mwanadamu, hata hivyo likiisha kuthibitika, hakuna mtu alibatilishaye, wala kuliongeza neno. 16#Mwa 12:7; 13:15; 17:7; 22:18; 24:7 Basi ahadi zilinenwa kwa Abrahamu na kwa mzao wake. Hasemi, Kwa wazawa, kana kwamba ni wengi, bali kana kwamba ni mmoja, Kwa mzao wako, yaani, Kristo. 17#Kut 12:40 Nisemalo ni hili; agano lililothibitishwa kwanza na Mungu, torati iliyotokea miaka mia nne na thelathini baadaye hailitangui, hata kuibatilisha ile ahadi. 18#Rum 4:14; 11:6 Kwa maana urithi ukiwa kwa sheria, hauwi tena kwa ahadi; lakini Mungu alimkirimia Abrahamu kwa njia ya ahadi.
Kusudi ya Torati
19 # Rum 5:20; Ebr 2:2; Mdo 7:38,53 Torati ni nini basi? Iliingizwa kwa sababu ya makosa, hadi aje huyo mzao aliyepewa ile ahadi; iliamriwa kwa utumishi wa malaika kwa mkono wa mjumbe. 20Basi aliye mjumbe si mjumbe wa mmoja; bali Mungu ni mmoja. 21#Rum 8:2-4 Basi je! Torati haipatani na ahadi za Mungu? La hasha! Kwa kuwa, kama ingalitolewa sheria iwezayo kuhuisha, hakika haki ingalipatikana kwa sheria. 22#Rum 3:9-19; 11:32 Lakini andiko limeyafunga yote chini ya nguvu ya dhambi, makusudi hao waaminio wapewe ile ahadi kwa imani ya Yesu Kristo.
23 # Gal 4:3; 1 Pet 1:5 Lakini kabla ya kuja ile imani tulikuwa tumewekwa chini ya sheria, tumefungwa mpaka ije ile imani itakayofunuliwa. 24Hivyo torati imekuwa kiongozi kutuleta kwa Kristo, ili tuhesabiwe haki kwa imani. 25#Rum 10:4 Lakini, iwapo imani imekuja, hatupo tena chini ya kiongozi. 26#Yn 1:12; Rum 8:17 Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa Mungu kwa njia ya imani katika Kristo Yesu. 27#Rum 6:3; 13:14 Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo. 28#Rum 10:12; 1 Kor 12:13 Hakuna Myahudi wala Mgiriki. Hakuna mtumwa wala huru. Hakuna mwanamume wala mwanamke. Maana ninyi nyote mmekuwa wamoja katika Kristo Yesu. 29#Rum 4:13; 9:7 Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Abrahamu, na warithi kulingana na ahadi.

Iliyochaguliwa sasa

Wagalatia 3: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha