Ezra 2:1-70
Ezra 2:1-70 Biblia Habari Njema (BHN)
Wafuatao ni watu wa mkoani waliotoka utumwani ambao Nebukadneza mfalme wa Babuloni aliwapeleka mateka Babuloni, wakarudi mjini Yerusalemu na nchini Yuda. Kila mtu alirudi mjini kwake. Viongozi wao walikuwa Zerubabeli, Yeshua, Nehemia, Seraya, Reelaya, Mordekai, Bilshani, Mispari, Bigwai, Rehumu na Baana. Ifuatayo ni idadi ya watu wote wa koo za Israeli waliorudi kutoka uhamishoni: Wa ukoo wa Paroshi: 2,172; wa ukoo wa Shefatia: 372; wa ukoo wa Ara: 775; wa ukoo wa Pahath-moabu, yaani wazawa wa Yeshua na Yoabu: 2,812; wa ukoo wa Elamu: 1,254; wa ukoo wa Zatu: 945; wa ukoo wa Zakai: 760; wa ukoo wa Bani: 842; wa ukoo wa Bebai: 623; wa ukoo wa Azgadi: 1,222; wa ukoo wa Adonikamu: 666; wa ukoo wa Bigwai: 2,056; wa ukoo wa Adini: 454; wa ukoo wa Ateri, yaani Hezekia: 98; wa ukoo wa Besai: 323; wa ukoo wa Yora: 112; wa ukoo wa Hashumu: 223; wa ukoo wa Gibari: 95. Watu wa mji wa Bethlehemu: 123; wa mji wa Netofa: 56; wa mji wa Anathothi: 128; wa mji wa Azmawethi: 42; wa mji wa Kiriath-yearimu, wa Kefira na wa Beerothi: 743; wa mji wa Rama na wa Geba: 621; wa mji wa Mikmashi: 122; wa mji wa Betheli na Ai: 223; wa mji wa Nebo: 52; wa mji wa Magbishi: 156; wa mji wa Elamu wa pili: 1,254; wa mji wa Harimu: 320; wa mji wa Lodi, Hadidi na wa Ono: 725; wa mji wa Yeriko: 345; wa mji wa Senaa: 3,630. Ifuatayo ni idadi ya makuhani waliorudi kutoka uhamishoni: Makuhani wa ukoo wa Yedaya, waliokuwa wazawa wa Yeshua: 673; wa ukoo wa Imeri: 1,052; wa ukoo wa Pashuri: 1,247; wa ukoo wa Harimu: 1,017. Walawi wa ukoo wa Yeshua na wa Kadmieli, wazawa wa Hodavia waliorudi kutoka uhamishoni walikuwa 74. Waimbaji (wazawa wa Asafu), walikuwa 128. Walinzi (wazawa wa Shalumu, wa Ateri, wa Talmoni, wa Akubu, wa Hatita na wa Shobai), walikuwa 139. Koo za watumishi wa hekalu waliorudi kutoka uhamishoni zilikuwa: Ukoo wa Siha, wa Hasufa, wa Tabaothi, ukoo wa Kerosi, wa Siaha, wa Padoni, ukoo wa Lebana, wa Hagaba, wa Akubu, ukoo wa Hagabu, wa Shamlai, wa Hanani, ukoo wa Gideli, wa Gahari, wa Reaya, ukoo wa Resini, wa Nekoda, wa Gazamu, ukoo wa Uza, wa Pasea, wa Besai, ukoo wa Asna, wa Meunimu, wa Nefisimu, ukoo wa Bakbuki, wa Hakufa, wa Harhuri, ukoo wa Basluthi, wa Mehida, wa Harsha, ukoo wa Barkosi, wa Sisera, wa Tema, ukoo wa Nezia na wa Hatifa. Koo za wazawa wa watumishi wa Solomoni waliorudi kutoka uhamishoni zilikuwa, ukoo wa Sotai, wa Hasoferethi, wa Perudha, ukoo wa Yaala, wa Darkoni, wa Gideli, ukoo wa Shefatia, wa Hatili, wa Pokereth-hasebaimu na wa Ami. Nao watumishi wote wa hekalu na wazawa wa watumishi wa Solomoni waliorudi kutoka uhamishoni walikuwa watu 392. Watu wa miji ifuatayo, pia walirudi: Wa mji wa Tel-mela, wa Tel-harsha, wa Kerubu, wa Adani na wa Imeri, ila hawakuweza kuthibitisha kuwa walikuwa wazawa wa Waisraeli. Wao walikuwa watu wa ukoo wa Delaya wa Tobia na wa Nekoda, jumla watu 652. Watu wa koo zifuatazo za makuhani pia walirudi: Ukoo wa Habaya, wa Hakosi na wa Barzilai. Huyo Barzilai alikuwa ameoa binti Barzilai wa Gileadi, naye pia akaitwa Barzilai. Hao walitafuta orodha yao katika kumbukumbu za koo, lakini hawakuonekana humo. Kwa hiyo hawakuruhusiwa kushika ukuhani kwani walihesabiwa kuwa najisi. Mtawala akawaambia kuwa hawaruhusiwi kushiriki chakula kitakatifu sana, mpaka awepo kuhani atakayeweza kutoa kauli ya Urimu na Thumimu. Watu wote waliorudi kutoka uhamishoni jumla yao ilikuwa 42,360; mbali na hao, kulikuwa na watumishi wanaume na wanawake 7337; na walikuwa na waimbaji wanaume na wanawake, wote 200. Walikuwa na farasi 736, nyumbu 245, ngamia 435, na punda 6,720. Watu hao waliotoka uhamishoni, walipofika kwenye nyumba ya Mwenyezi-Mungu mjini Yerusalemu, baadhi ya viongozi wa koo hizo walitoa matoleo ya hiari ili kusaidia ujenzi wa nyumba ya Mungu katika Yerusalemu. Walitoa kila mtu kadiri ya uwezo wake kwa ajili ya kazi hii. Jumla ya matoleo hayo ilikuwa kilo 500 za dhahabu, kilo 2,800 za fedha na mavazi 100 kwa ajili ya makuhani. Basi, makuhani, Walawi na baadhi ya watu wengine wakaanza kuishi mjini Yerusalemu na katika vitongoji vyake. Nao waimbaji, walinzi wa hekalu na watumishi wa hekalu wakaanza kuishi katika miji yao; Waisraeli wote waliishi katika miji yao.
Ezra 2:1-70 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Basi hawa ndio watu wa mkoa, waliokwea kutoka katika ule uhamisho wa hao waliokuwa wamechukuliwa, ambao Nebukadneza, mfalme wa Babeli, aliwachukua mateka mpaka Babeli, nao wakarudi Yerusalemu na Yuda, kila mtu mjini kwake; ndio hawa waliokuja pamoja na Zerubabeli, Yoshua, Nehemia, Seraya, Reelaya, Mordekai, Bilshani, Mispari, Bigwai, Rehumu, na Baana. Hii ndiyo hesabu ya watu wa Israeli; wazawa wa Paroshi, elfu mbili mia moja sabini na wawili. Wazawa wa Shefatia, mia tatu sabini na wawili. Wazawa wa Ara, mia saba sabini na watano. Wazawa wa Pahath-Moabu, wazawa wa Yeshua na Yoabu, elfu mbili mia nane na kumi na wawili. Wazawa wa Elamu, elfu moja mia mbili hamsini na wanne. Wazawa wa Zatu, mia tisa arubaini na watano. Wazawa wa Zakai, mia saba na sitini. Wazawa wa Binui, mia sita arubaini na wawili. Wazawa wa Bebai, mia sita ishirini na watatu. Wazawa wa Azgadi, elfu moja mia mbili ishirini na wawili. Wazawa wa Adonikamu, mia sita sitini na sita. Wazawa wa Bigwai, elfu mbili hamsini na sita. Wazawa wa Adini, mia nne hamsini na wanne. Wazawa wa Ateri, wazawa wa Hezekia, tisini na wanane. Wazawa wa Besai, mia tatu ishirini na watatu. Wazawa wa Harifu, mia moja na kumi na wawili. Wazawa wa Hashumu, mia mbili ishirini na watatu. Watu wa Gibari, tisini na watano. Watu wa Bethlehemu, mia moja ishirini na watatu. Watu wa Netofa, hamsini na sita. Watu wa Anathothi, mia moja ishirini na wanane. Watu wa Beth-Azmawethi, arubaini na wawili. Watu wa Kiriath-yearimu, na Kefira, na Beerothi, mia saba arubaini na watatu. Watu wa Rama na Geba, mia sita ishirini na mmoja. Watu wa Mikmashi, mia moja ishirini na wawili. Watu wa Betheli, na Ai, mia mbili ishirini na watatu. Watu wa Nebo, hamsini na wawili. Watu wa Magbishi, mia moja hamsini na sita. Watu wa Elamu wa pili, elfu moja mia mbili hamsini na wanne. Watu wa Harimu, mia tatu na ishirini. Watu wa Lodi, na Hadidi, na Ono, mia saba ishirini na watano. Watu wa Yeriko, mia tatu arubaini na watano. Watu wa Senaa, elfu tatu mia sita na thelathini. Makuhani; wazawa wa Yedaya, wa ukoo wa Yeshua, mia tisa sabini na watatu. Wazawa wa Imeri, elfu moja hamsini na wawili. Wazawa wa Pashuri, elfu moja mia mbili arubaini na saba. Wazawa wa Harimu, elfu moja na kumi na saba. Walawi; wazawa wa Yeshua, wazawa wa Kadmieli wa wawazawa wa Hodavia, sabini na wanne. Waimbaji; wazawa wa Asafu, mia moja ishirini na wanane. Akina bawabu; wazawa wa Shalumu, wazawa wa Ateri, wazawa wa Talmoni, wazawa wa Akubu, wazawa wa Hatita, wazawa wa Shobai; jumla yao ni mia moja thelathini na tisa. Wanethini; wazawa wa Siha, wazawa wa Hasufa, wazawa wa Tabaothi; wazawa wa Kerosi, wazawa wa Siaha, wazawa wa Padoni; wazawa wa Lebana, wazawa wa Hagaba, wazawa wa Akubu; wazawa wa Hagabu, wazawa wa Salmai, wazawa wa Hanani; wazawa wa Gideli, wazawa wa Gahari, wazawa wa Reaya; wazawa wa Resini, wazawa wa Nekoda, wazawa wa Gazamu; wazawa wa Uza, wazawa wa Pasea, wazawa wa Besai; wazawa wa Asna, wazawa wa Meunimu, wazawa wa Nefusimu; wazawa wa Bakbuki, wazawa wa Hakufa, wazawa wa Harhuri; wazawa wa Basluthi, wazawa wa Mehida, wazawa wa Harsha; wazawa wa Barkosi, wazawa wa Sisera, wazawa wa Tema; wazawa wa Nesia, wazawa wa Hatifa. Wazawa wa watumishi wa Sulemani; wazawa wa Sotai, wazawa wa Soferethi, wazawa wa Peruda; wazawa wa Yaala, wazawa wa Darkoni, wazawa wa Gideli; wazawa wa Shefatia, wazawa wa Hatili, wazawa wa Pokereth-Sebaimu, wazawa wa Amoni. Wanethini wote, pamoja na wazawa wa watumishi wa Sulemani, walikuwa mia tatu tisini na wawili. Na hawa ndio watu waliokwea kutoka Tel-mela, na Tel-harsha, na Kerubu, na Adani, na Imeri; lakini hawakuweza kuonesha koo za baba zao, wala kizazi chao, kwamba walikuwa wa Israeli; wazawa wa Delaya, wazawa wa Tobia na wazawa wa Nekoda, mia sita hamsini na wawili. Tena wa makuhani; wazawa wa Habaya, wazawa wa Hakosi, wazawa wa Barzilai, yule aliyeoa mmojawapo wa binti Barzilai, Mgileadi, akaitwa kwa jina lao. Hao waliitafuta orodha yao miongoni mwa wale waliohesabiwa kwa nasaba, wasionekane; kwa hiyo walihesabiwa kuwa na unajisi. Na huyo Tirshatha akawaambia kwamba wasile katika vitu vitakatifu sana, hata atakaposimama kuhani mwenye Urimu na Thumimu. Basi hilo kusanyiko lote nzima, jumla yake ilikuwa watu elfu arubaini na mbili na mia tatu na sitini, tena, zaidi ya hao, kulikuwa na watumishi wao wa kiume na wa kike, ambao walikuwa elfu saba, na mia tatu na thelathini na saba; nao walikuwa na waimbaji wa kiume na wa kike mia mbili. Farasi wao walikuwa mia saba thelathini na sita; nyumbu wao, mia mbili arubaini na watano; ngamia wao, mia nne thelathini na watano; punda wao elfu sita, mia saba na ishirini. Na baadhi ya wakuu wa koo za baba zao, hapo walipoifikia nyumba ya BWANA, iliyoko Yerusalemu, walitoa mali kwa ukarimu kwa ajili ya nyumba ya Mungu, ili kuisimamisha mahali pake; wakatoa kadiri walivyoweza, na kutia katika hazina ya kazi hiyo, darkoni za dhahabu elfu sitini na moja, na mane za fedha elfu tano, na mavazi mia moja ya makuhani. Hivyo makuhani, na Walawi, na baadhi ya watu, na waimbaji, na mabawabu, na Wanethini, wakakaa mijini mwao, naam, Israeli wote wakakaa mijini mwao.
Ezra 2:1-70 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Basi hawa ndio wana wa wilaya, waliokwea kutoka katika ule uhamisho wa hao waliokuwa wamechukuliwa, ambao Nebukadneza, mfalme wa Babeli, aliwachukua mateka mpaka Babeli, nao wakarudi Yerusalemu na Yuda, kila mtu mjini kwake; ndio hawa waliokuja pamoja na Zerubabeli, Yoshua, Nehemia, Seraya, Reelaya, Mordekai, Bilshani, Mispari, Bigwai, Rehumu, na Baana. Hii ndiyo hesabu ya wanaume wa watu wa Israeli; wana wa Paroshi, elfu mbili mia moja sabini na wawili. Wana wa Shefatia, mia tatu sabini na wawili. Wana wa Ara, mia saba sabini na watano. Wana wa Pahath-Moabu, wa wana wa Yeshua na Yoabu, elfu mbili mia nane na kumi na wawili. Wana wa Elamu, elfu moja mia mbili hamsini na wanne. Wana wa Zatu, mia kenda arobaini na watano. Wana wa Zakai, mia saba na sitini. Wana wa Binui, mia sita arobaini na wawili. Wana wa Bebai, mia sita ishirini na watatu. Wana wa Azgadi, elfu moja mia mbili ishirini na wawili. Wana wa Adonikamu, mia sita sitini na sita. Wana wa Bigwai, elfu mbili hamsini na sita. Wana wa Adini, mia nne hamsini na wanne. Wana wa Ateri, wa wana wa Hezekia, tisini na wanane. Wana wa Besai, mia tatu ishirini na watatu. Wana wa Harifu, mia moja na kumi na wawili. Wana wa Hashumu, mia mbili ishirini na watatu. Watu wa Gibeoni, tisini na watano. Watu wa Bethlehemu, mia ishirini na watatu. Watu wa Netofa, hamsini na sita. Watu wa Anathothi, mia ishirini na wanane. Watu wa Beth-Azmawethi, arobaini na wawili. Watu wa Kiriath-yearimu, na Kefira, na Beerothi, mia saba arobaini na watatu. Watu wa Rama na Geba, mia sita ishirini na mmoja. Watu wa Mikmashi, mia moja ishirini na wawili. Watu wa Betheli, na Ai, mia mbili ishirini na watatu. Watu wa Nebo, hamsini na wawili. Watu wa Magbishi, mia moja hamsini na sita. Watu wa Elamu wa pili, elfu moja mia mbili hamsini na wanne. Watu wa Harimu, mia tatu na ishirini. Watu wa Lodi, na Hadidi, na Ono, mia saba ishirini na watano. Watu wa Yeriko, mia tatu arobaini na watano. Watu wa Senaa, elfu tatu mia sita na thelathini. Makuhani; wana wa Yedaya, wa mbari ya Yeshua, mia kenda sabini na watatu. Wana wa Imeri, elfu moja hamsini na wawili. Wana wa Pashuri, elfu moja mia mbili arobaini na saba. Wana wa Harimu, elfu moja na kumi na saba. Walawi; wana wa Yeshua, na wana wa Kadmieli wa wana wa Hodavia, sabini na wanne. Waimbaji; wana wa Asafu, mia moja ishirini na wanane. Akina bawabu; wana wa Shalumu, wana wa Ateri, wana wa Talmoni, wana wa Akubu, wana wa Hatita, wana wa Shobai; jumla yao ni mia moja thelathini na kenda. Wanethini; wana wa Siha, wana wa Hasufa, wana wa Tabaothi; wana wa Kerosi, wana wa Siaha, wana wa Padoni; wana wa Lebana, wana wa Hagaba, wana wa Akubu; wana wa Hagabu, wana wa Salmai, wana wa Hanani; wana wa Gideli, wana wa Gahari, wana wa Reaya; wana wa Resini, wana wa Nekoda, wana wa Gazamu; wana wa Uza, wana wa Pasea, wana wa Besai; wana wa Asna, wana wa Meunimu, wana wa Nefusimu; wana wa Bakbuki, wana wa Hakufa, wana wa Harhuri; wana wa Basluthi, wana wa Mehida, wana wa Harsha; wana wa Barkosi, wana wa Sisera, wana wa Tema; wana wa Nesia, wana wa Hatifa. Wa watumwa wa Sulemani; wana wa Sotai, wana wa Soferethi, wana wa Peruda; wana wa Yaala, wana wa Darkoni, wana wa Gideli; wana wa Shefatia, wana wa Hatili, wana wa Pokereth-Sebaimu, wana wa Amoni. Wanethini wote, pamoja na watumwa wa Sulemani, walikuwa mia tatu tisini na wawili. Na hawa ndio watu waliokwea kutoka Tel-mela, na Tel-harsha, na Kerubu, na Adani, na Imeri; walakini hawakuweza kuonyesha mbari za baba zao, wala kizazi chao, kwamba walikuwa wa Israeli; wana wa Delaya, wana wa Tobia, wana wa Nekoda, mia sita hamsini na wawili. Tena wa makuhani; wana wa Habaya, wana wa Hakosi, wana wa Barzilai, yule aliyeoa mmojawapo wa binti Barzilai, Mgileadi, akaitwa kwa jina lao. Hao waliitafuta orodha yao miongoni mwa wale waliohesabiwa kwa nasaba, wasionekane; kwa hiyo walihesabiwa kuwa na unajisi. Na huyo Tirshatha akawaambia kwamba wasile katika vitu vitakatifu sana, hata atakaposimama kuhani mwenye Urimu na Thumimu. Basi hilo kusanyiko lote zima, jumla yake ilikuwa watu arobaini na mbili elfu na mia tatu na sitini, tena, zaidi ya hao, kulikuwa na watumishi wao waume kwa wake, ambao walikuwa saba elfu, na mia tatu na thelathini na saba; nao walikuwa na waimbaji waume kwa wake mia mbili. Farasi zao walikuwa mia saba thelathini na sita; nyumbu zao, mia mbili arobaini na watano; ngamia zao, mia nne thelathini na watano; punda zao elfu sita, na mia saba na ishirini. Na baadhi ya wakuu wa mbari za baba zao, hapo walipoifikilia nyumba ya BWANA, iliyoko Yerusalemu, walitoa mali kwa ukarimu kwa ajili ya nyumba ya Mungu, ili kuisimamisha mahali pake; wakatoa kadiri walivyoweza, na kutia katika hazina ya kazi hiyo, darkoni za dhahabu sitini na moja elfu, na mane za fedha elfu tano, na mavazi mia ya makuhani. Hivyo makuhani, na Walawi, na baadhi ya watu, na waimbaji, na mabawabu, na Wanethini, wakakaa mijini mwao, naam, Israeli wote wakakaa mijini mwao.
Ezra 2:1-70 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Basi hawa ndio watu wa jimbo waliotoka uhamishoni, ambao Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuwa amewachukua mateka hadi Babeli (walirudi Yerusalemu na Yuda, kila mmoja kwenye mji wake, wakiwa wamefuatana na Zerubabeli, Yeshua, Nehemia, Seraya, Reelaya, Mordekai, Bilshani, Mispari, Bigwai, Rehumu na Baana): Orodha ya wanaume kati ya watu wa Israeli ilikuwa: wazao wa Paroshi, elfu mbili mia moja sabini na wawili (2,172); wazao wa Shefatia, mia tatu sabini na wawili (372); wazao wa Ara, mia saba sabini na watano (775); wazao wa Pahath-Moabu (wa jamaa ya Yeshua na Yoabu), elfu mbili mia nane na kumi na wawili (2,812); wazao wa Elamu, elfu moja mia mbili hamsini na wanne (1,254); wazao wa Zatu, mia tisa arobaini na watano (945); wazao wa Zakai, mia saba na sitini (760); wazao wa Bani, mia sita arobaini na wawili (642); wazao wa Bebai, mia sita ishirini na watatu (623); wazao wa Azgadi, elfu moja mia mbili ishirini na wawili (1,222); wazao wa Adonikamu, mia sita sitini na sita (666); wazao wa Bigwai, elfu mbili hamsini na sita (2,056); wazao wa Adini, mia nne hamsini na wanne (454); wazao wa Ateri (kupitia Hezekia), tisini na nane (98); wazao wa Besai, mia tatu ishirini na watatu (323); wazao wa Yora, mia moja na kumi na wawili (112); wazao wa Hashumu, mia mbili na ishirini na watatu (223); wazao wa Gibari, tisini na watano (95); watu wa Bethlehemu, mia moja ishirini na watatu (123); watu wa Netofa, hamsini na sita (56); watu wa Anathothi, watu mia moja ishirini na nane (128); watu wa Azmawethi, arobaini na wawili (42); wazao wa Kiriath-Yearimu, Kefira na Beerothi, mia saba arobaini na watatu (743); wazao wa Rama na Geba, mia sita ishirini na mmoja (621); watu wa Mikmashi, mia moja ishirini na wawili (122); watu wa Betheli na Ai, mia mbili na ishirini na watatu (223); wazao wa Nebo, hamsini na wawili (52); wazao wa Magbishi, mia moja hamsini na sita (156); wazao wa Elamu ile ingine, elfu moja mia mbili hamsini na wanne (1,254); wazao wa Harimu, mia tatu na ishirini (320); wazao wa Lodi, Hadidi na Ono, mia saba ishirini na watano (725); wazao wa Yeriko, mia tatu arobaini na watano (345); wazao wa Senaa, elfu tatu mia sita na thelathini (3,630). Makuhani: wazao wa Yedaya (kwa jamaa ya Yeshua), mia tisa sabini na watatu (973); wazao wa Imeri, elfu moja hamsini na wawili (1,052); wazao wa Pashuri, elfu moja mia mbili arobaini na saba (1,247); wazao wa Harimu, elfu moja na kumi na saba (1,017). Walawi: wazao wa Yeshua na Kadmieli (kupitia jamaa ya Hodavia), sabini na wanne (74). Waimbaji: wazao wa Asafu, mia moja ishirini na nane (128). Mabawabu wa lango la Hekalu: wazao wa Shalumu, Ateri, Talmoni, Akubu, Hatita na Shobai, mia moja thelathini na tisa (139). Watumishi wa Hekalu: wazao wa Siha, Hasufa, Tabaothi, wazao wa Kerosi, Siaha, Padoni, wazao wa Lebana, Hagaba, Akubu, wazao wa Hagabu, Shalmai, Hanani, wazao wa Gideli, Gahari, Reaya, wazao wa Resini, Nekoda, Gazamu, wazao wa Uza, Pasea, Besai, wazao wa Asna, Meunimu, Nefusimu, wazao wa Bakbuki, Hakufa, Harhuri, wazao wa Basluthi, Mehida, Harsha, wazao wa Barkosi, Sisera, Tema, wazao wa Nesia na Hatifa. Wazao wa watumishi wa Sulemani: wazao wa Sotai, Hasaferethi, Peruda, wazao wa Yaala, Darkoni, Gideli, wazao wa Shefatia, Hatili, Pokereth-Hasebaimu na Ami. Watumishi wa Hekalu, na wazao wa watumishi wa Sulemani, mia tatu tisini na wawili (392). Wafuatao walikuja kutoka miji ya Tel-Mela, Tel-Harsha, Kerubu, Adoni na Imeri, lakini hawakuweza kuthibitisha kwamba jamaa zao zilikuwa uzao wa Israeli: wazao wa Delaya, Tobia na Nekoda, mia sita hamsini na wawili (652). Kutoka miongoni mwa makuhani: Wazao wa Hobaya, Hakosi, Barzilai (mtu aliyemwoa binti Barzilai Mgileadi, naye akaitwa kwa jina hilo). Hawa walitafuta orodha za jamaa zao, lakini hawakuonekana humo, kwa hiyo waliondolewa ukuhani kwa kuwa walihesabiwa kuwa najisi. Mtawala aliagiza kuwa wasile chochote miongoni mwa vyakula vitakatifu hadi kuwe kuhani atakayehudumu kwa Urimu na Thumimu. Jumla ya watu wote waliorudi walikuwa elfu arobaini na mbili na mia tatu na sitini (42,360); tena zaidi ya hao walikuwa na watumwa wa kiume na wa kike elfu saba, mia tatu na thelathini na saba (7,337); pia walikuwa na waimbaji wanaume na wanawake mia mbili. Walikuwa na farasi mia saba thelathini na sita (736), nyumbu mia mbili arobaini na watano (245), ngamia mia nne thelathini na watano (435), na punda elfu sita, mia saba na ishirini (6,720). Walipofika kwenye nyumba ya BWANA huko Yerusalemu, baadhi ya viongozi wa jamaa walitoa sadaka za hiari kwa ajili ya kujenga upya nyumba ya Mungu katika eneo lake. Wakatoa kwa kadiri ya uwezo wao na kutia katika hazina darkoni elfu sitini na moja za dhahabu, mane elfu tano za fedha, na mavazi mia moja ya ukuhani kwa ajili ya kazi hiyo. Makuhani, Walawi, waimbaji, mabawabu, na watumishi wa Hekalu waliishi katika miji yao wenyewe, pamoja na baadhi ya watu wengine, nao Waisraeli waliosalia waliishi katika miji yao.