Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ezr 2

2
Watu Waliorudi kutoka Uhamishoni
1 # Ezr 5:8; 6:2; Est 1:1; 8:9; 2 Fal 24:14-16; 2 Nya 36:20 Basi hawa ndio wana wa wilaya, waliokwea kutoka katika ule uhamisho wa hao waliokuwa wamechukuliwa, ambao Nebukadneza, mfalme wa Babeli, aliwachukua mateka mpaka Babeli, nao wakarudi Yerusalemu na Yuda, kila mtu mjini kwake; 2ndio hawa waliokuja pamoja na Zerubabeli, Yoshua, Nehemia, Seraya, Reelaya, Mordekai, Bilshani, Mispari, Bigwai, Rehumu, na Baana. Hii ndiyo hesabu ya wanaume wa watu wa Israeli; 3wana wa Paroshi, elfu mbili mia moja sabini na wawili. 4Wana wa Shefatia, mia tatu sabini na wawili. 5#Neh 6:18Wana wa Ara, mia saba sabini na watano. 6Wana wa Pahath-Moabu, wa wana wa Yeshua na Yoabu, elfu mbili mia nane na kumi na wawili. 7Wana wa Elamu, elfu moja mia mbili hamsini na wanne. 8Wana wa Zatu, mia kenda arobaini na watano. 9Wana wa Zakai, mia saba na sitini. 10Wana wa Binui, mia sita arobaini na wawili. 11Wana wa Bebai, mia sita ishirini na watatu. 12Wana wa Azgadi, elfu moja mia mbili ishirini na wawili. 13#Ezr 7:18; 8:13Wana wa Adonikamu, mia sita sitini na sita. 14Wana wa Bigwai, elfu mbili hamsini na sita. 15Wana wa Adini, mia nne hamsini na wanne. 16Wana wa Ateri, wa wana wa Hezekia, tisini na wanane. 17Wana wa Besai, mia tatu ishirini na watatu. 18Wana wa Harifu, mia moja na kumi na wawili. 19Wana wa Hashumu, mia mbili ishirini na watatu.
20 # Yos 9:17; 2 Sam 21:2 Watu wa Gibeoni, tisini na watano. 21#Mwa 35:19; Mt 2:6; Rut 1:19; 1 Nya 2:51Watu wa Bethlehemu, mia ishirini na watatu. 22Watu wa Netofa, hamsini na sita. 23Watu wa Anathothi, mia ishirini na wanane. 24Watu wa Beth-Azmawethi, arobaini na wawili. 25Watu wa Kiriath-yearimu, na Kefira, na Beerothi, mia saba arobaini na watatu. 26#Yos 18:25; 1 Sam 7:17; 15:34; Yer 31:15Watu wa Rama na Geba, mia sita ishirini na mmoja. 27Watu wa Mikmashi, mia moja ishirini na wawili. 28Watu wa Betheli, na Ai, mia mbili ishirini na watatu. 29Watu wa Nebo, hamsini na wawili. 30Watu wa Magbishi, mia moja hamsini na sita. 31#Ezr 2:7Watu wa Elamu wa pili, elfu moja mia mbili hamsini na wanne. 32Watu wa Harimu, mia tatu na ishirini. 33Watu wa Lodi, na Hadidi, na Ono, mia saba ishirini na watano. 34#Kum 34:3; 2 Nya 28:15Watu wa Yeriko, mia tatu arobaini na watano. 35Watu wa Senaa, elfu tatu mia sita na thelathini.
36 # 1 Nya 9:10; 24:7 Makuhani; wana wa Yedaya, wa mbari ya Yeshua, mia kenda sabini na watatu. 37#1 Nya 24:14; Ezr 10:20Wana wa Imeri, elfu moja hamsini na wawili. 38#1 Nya 9:12; Ezr 10:22Wana wa Pashuri, elfu moja mia mbili arobaini na saba. 39#1 Nya 24:8Wana wa Harimu, elfu moja na kumi na saba.
40 # Ezr 3:9 Walawi; wana wa Yeshua, na wana wa Kadmieli wa wana wa Hodavia, sabini na wanne.
41Waimbaji; wana wa Asafu, mia moja ishirini na wanane.
42Akina bawabu; wana wa Shalumu, wana wa Ateri, wana wa Talmoni, wana wa Akubu, wana wa Hatita, wana wa Shobai; jumla yao ni mia moja thelathini na kenda.
43 # 1 Nya 9:2 Wanethini; wana wa Siha, wana wa Hasufa, wana wa Tabaothi; 44wana wa Kerosi, wana wa Siaha, wana wa Padoni; 45wana wa Lebana, wana wa Hagaba, wana wa Akubu; 46wana wa Hagabu, wana wa Salmai, wana wa Hanani; 47wana wa Gideli, wana wa Gahari, wana wa Reaya; 48wana wa Resini, wana wa Nekoda, wana wa Gazamu; 49wana wa Uza, wana wa Pasea, wana wa Besai; 50wana wa Asna, wana wa Meunimu, wana wa Nefusimu; 51wana wa Bakbuki, wana wa Hakufa, wana wa Harhuri; 52wana wa Basluthi, wana wa Mehida, wana wa Harsha; 53wana wa Barkosi, wana wa Sisera, wana wa Tema; 54wana wa Nesia, wana wa Hatifa.
55 # 1 Fal 9:21 Wa watumwa wa Sulemani; wana wa Sotai, wana wa Soferethi, wana wa Peruda; 56wana wa Yaala, wana wa Darkoni, wana wa Gideli; 57wana wa Shefatia, wana wa Hatili, wana wa Pokereth-Sebaimu, wana wa Amoni. 58#Yos 9:21,27; 1 Nya 9:2; Ezr 7:7; 1 Fal 9:21Wanethini wote, pamoja na watumwa wa Sulemani, walikuwa mia tatu tisini na wawili.
59Na hawa ndio watu waliokwea kutoka Tel-mela, na Tel-harsha, na Kerubu, na Adani, na Imeri; walakini hawakuweza kuonyesha mbari za baba zao, wala kizazi chao, kwamba walikuwa wa Israeli; 60wana wa Delaya, wana wa Tobia, wana wa Nekoda, mia sita hamsini na wawili. 61#1 Fal 2:7Tena wa makuhani; wana wa Habaya, wana wa Hakosi, wana wa Barzilai, yule aliyeoa mmojawapo wa binti Barzilai, Mgileadi, akaitwa kwa jina lao. 62#Hes 3:10Hao waliitafuta orodha yao miongoni mwa wale waliohesabiwa kwa nasaba, wasionekane; kwa hiyo walihesabiwa kuwa na unajisi. 63#Neh 8:9; Law 22:2,10,15,16; Hes 18:9-11; Kut 28:30Na huyo Tirshatha#2:63 Tirshatha ni jina la heshima aliloitwa liwali. akawaambia kwamba wasile katika vitu vitakatifu sana, hata atakaposimama kuhani mwenye Urimu na Thumimu.
64 # Isa 10:22 Basi hilo kusanyiko lote zima, jumla yake ilikuwa watu arobaini na mbili elfu na mia tatu na sitini, 65tena, zaidi ya hao, kulikuwa na watumishi wao waume kwa wake, ambao walikuwa saba elfu, na mia tatu na thelathini na saba; nao walikuwa na waimbaji waume kwa wake mia mbili. 66Farasi zao walikuwa mia saba thelathini na sita; nyumbu zao, mia mbili arobaini na watano; 67ngamia zao, mia nne thelathini na watano; punda zao elfu sita, na mia saba na ishirini. 68#Kut 25:2Na baadhi ya wakuu wa mbari za baba zao, hapo walipoifikilia nyumba ya BWANA, iliyoko Yerusalemu, walitoa mali kwa ukarimu kwa ajili ya nyumba ya Mungu, ili kuisimamisha mahali pake; 69wakatoa kadiri walivyoweza, na kutia katika hazina ya kazi hiyo, darkoni#2:69 Darkoni ni sarafu, thamani yake ni kama shilingi 21. za dhahabu sitini na moja elfu, na mane#2:69 Mane ya fedha ni kama shilingi 136. za fedha elfu tano, na mavazi mia ya makuhani. 70Hivyo makuhani, na Walawi, na baadhi ya watu, na waimbaji, na mabawabu, na Wanethini, wakakaa mijini mwao, naam, Israeli wote wakakaa mijini mwao.

Iliyochaguliwa sasa

Ezr 2: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha