Kutoka 2:23-25 - Compare All Versions
Kutoka 2:23-25 BHN (Biblia Habari Njema)
Baada ya muda mrefu, mfalme wa Misri akafa. Waisraeli wakapiga kite na kulia kutokana na hali yao ya utumwa, na kilio chao kikamfikia Mungu juu. Mungu akasikia kilio chao, naye akakumbuka agano alilofanya na Abrahamu, na Isaka na Yakobo. Mungu aliwaangalia Waisraeli, akaona kuwa hali yao ni mbaya.
Kutoka 2:23-25 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata baada ya siku zile nyingi mfalme wa Misri akafa; wana wa Israeli wakaugua kwa sababu ya ule utumwa, wakalia; kilio chao kikafika juu kwa Mungu kwa sababu ya ule utumwa. Mungu akasikia kuugua kwao, Mungu akakumbuka agano lake alilolifanya na Ibrahimu na Isaka na Yakobo. Mungu akawaona wana wa Israeli, na Mungu akawaangalia.
Kutoka 2:23-25 SRUV (Swahili Revised Union Version)
Na kisha baada ya muda, yule mfalme wa Misri akafa; wana wa Israeli wakaugua kwa sababu ya ule utumwa, wakalia; kilio chao kikafika juu kwa Mungu kwa sababu ya ule utumwa. Mungu akasikia kuugua kwao, Mungu akakumbuka agano lake alilolifanya na Abrahamu na Isaka na Yakobo. Mungu akawaona wana wa Israeli, na Mungu akawaangalia.
Kutoka 2:23-25 NEN (Neno)
Baada ya muda mrefu, mfalme wa Misri akafa. Waisraeli wakalia kwa huzuni katika utumwa wao, walilia na kilio chao cha kutaka msaada kwa ajili ya utumwa kikamfikia Mungu. Mungu akasikia kilio chao cha huzuni, akakumbuka agano alilofanya na Abrahamu pamoja na Isaka na Yakobo. Kwa hiyo Mungu akawaangalia Waisraeli na kuwahurumia.