Mhubiri 9:9-10
Mhubiri 9:9-10 Biblia Habari Njema (BHN)
Furahia maisha pamoja na mke wako umpendaye muda wote wa maisha yako ya bure ambayo Mungu amekujalia hapa duniani; maana hilo ndilo ulilopangiwa maishani, katika kazi zako hapa duniani. Kila unachotaka kufanya kifanye kwa nguvu zako zote, maana, hakuna kazi, wala wazo, wala maarifa, wala hekima huko kuzimu unakokwenda.
Mhubiri 9:9-10 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Uishi kwa furaha pamoja na mke umpendaye, siku zote za maisha yako ya ubatili, ulizopewa chini ya jua; siku zote za ubatili wako, kwa maana hiyo ni sehemu yako ya maisha; na katika kazi zako unazozifanya chini ya jua. Lolote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; kwa kuwa hakuna kazi, wala shauri, wala maarifa, wala hekima, huko kuzimu uendako wewe.
Mhubiri 9:9-10 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Uishi kwa furaha pamoja na mke umpendaye, siku zote za maisha yako ya ubatili, ulizopewa chini ya jua; siku zote za ubatili wako, kwa maana huo ni sehemu yako ya maisha; na katika taabu zako ulizozitaabika chini ya jua. Lo lote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; kwa kuwa hakuna kazi, wala shauri, wala maarifa, wala hekima, huko kuzimu uendako wewe.
Mhubiri 9:9-10 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Furahia maisha na mke wako, umpendaye, siku zote za maisha ya ubatili uliyopewa na Mungu chini ya jua, siku zote za ubatili. Kwa maana hili ndilo fungu lako katika maisha na katika kazi yako ya taabu chini ya jua. Lolote mkono wako upatalo kufanya, fanya kwa nguvu zako zote, kwa kuwa huko Kuzimu, unakoenda, hakuna kufanya kazi wala mipango wala maarifa wala hekima.