Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mhubiri 9

9
Yapokee maisha yalivyo
1 # 1 Sam 2:9; Ayu 5:8; Mit 16:3; Mhu 8:14; Isa 26:12; 2 Kor 3:5; 1 Pet 1:5 Na kwa ajili ya hayo yote, nikatia moyo wangu katika kuyachunguza haya; ya kuwa wenye haki, na wenye hekima, pamoja na matendo yao yote, wamo mkononi mwa Mungu; iwe ni upendo au iwe ni chuki, mwanadamu hajui; mambo yote yawapita. 2#Zab 73:3,12,13,17; Mal 3:15 Mambo yote yawatukia wote sawasawa; kuna tukio moja kwake mwenye haki na kwake asiye haki; kwa mtu mwema na kwa mtu mwovu; kwa mtu aliye safi na kwa mtu asiye safi; kwake yeye atoaye kafara na kwake asiyetoa kafara; kama alivyo huyo mwema ndivyo alivyo mwenye dhambi; yeye aapaye na yeye aogopaye kiapo. 3Baa hilo ni katika mambo yote yanayofanyika chini ya jua, ya kuwa wote wanalo tukio moja; naam, zaidi ya hayo, mioyo ya wanadamu imejaa maovu, na wazimu umo mioyoni mwao wakati walipo hai, na baadaye huenda kwa wafu. 4Kwa kuwa liko tumaini kwa yule aliyeambatana na wote walio hai; maana ni afadhali mbwa aliye hai kuliko simba aliyekufa; 5#Ayu 14:21; 7:8; Isa 63:16; 26:14; Zab 6:5 kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lolote, wala hawana tuzo tena; maana hata kumbukumbu lao limesahauliwa. 6Mapenzi yao na chuki yao, na husuda yao, imepotea yote pamoja; wala hawana sehemu tena katika jambo lolote lililofanyika chini ya jua.
7 # Mhu 8:15 Wewe nenda zako, ule chakula chako kwa furaha, unywe mvinyo yako kwa moyo wa kuchangamka; kwa kuwa Mungu amekwisha kuzikubali kazi zako. 8Mavazi yako na yawe meupe sikuzote; wala kichwa chako kisikose manukato. 9#Mhu 2:10,24 Uishi kwa furaha pamoja na mke umpendaye, siku zote za maisha yako ya ubatili, ulizopewa chini ya jua; siku zote za ubatili wako, kwa maana hiyo ni sehemu yako ya maisha; na katika kazi zako unazozifanya chini ya jua. 10Lolote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; kwa kuwa hakuna kazi, wala shauri, wala maarifa, wala hekima, huko kuzimu uendako wewe.
11 # Amo 2:14; Yer 9:23 Nikarudi, na kuona chini ya jua, ya kwamba si wenye mbio washindao katika michezo, wala si walio hodari washindao vitani, wala si wenye hekima wapatao chakula, wala si watu wa ufahamu wapatao mali, wala wenye ustadi wapatao upendeleo; lakini wakati na bahati huwapata wote. 12#Mhu 8:7; Mit 29:6; Lk 12:20; 1 The 5:3 Maana mwanadamu naye hajui wakati wake; kama samaki wanaokamatwa katika nyavu mbaya, na mfano wa ndege wanaonaswa mtegoni, kadhalika wanadamu hunaswa katika wakati mbaya, unapowaangukia kwa ghafla.
Hekima ni bora kuliko upumbavu
13Pia nimeona mfano huu wa hekima chini ya jua, nao ni kama hivi, tena kwangu mimi ulionekana kuwa neno kubwa. 14#2 Sam 20:16-22 Palikuwa na mji mdogo, uliokuwa na watu wachache ndani yake; akaja mfalme mkuu juu yake, akauhusuru, akajenga ngome kubwa ili kuupiga. 15Basi, kulikuwemo na mtu maskini mwenye hekima, naye kwa hekima yake akauokoa mji ule lakini hata hivyo hapakuwa na mtu yeyote aliyemkumbuka yule mtu maskini. 16#Mit 21:22; Mhu 7:19; Mk 6:2 Ndipo niliposema, Bora hekima kuliko nguvu; lakini hekima ya maskini hudharauliwa, wala maneno yake hayasikilizwi.
17 # Mwa 41:14; 2 Sam 20:17; Dan 5:10 Maneno ya wenye hekima yanenwayo taratibu husikiwa,
Zaidi ya mlio wake atawalaye katikati ya wapumbavu.
18 # Yos 7:1; 2 Fal 17:21; Rum 6:12,16-23 Hekima ndiyo bora kupita silaha za vita;
Lakini mkosaji mmoja huharibu mema mengi.

Iliyochaguliwa sasa

Mhubiri 9: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha