Wakolosai 1:19-20
Wakolosai 1:19-20 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kwa kuwa katika yeye ilipendeza utimilifu wote ukae; na kwa yeye kuvipatanisha vitu vyote na nafsi yake akiisha kufanya amani kwa damu ya msalaba wake; kwa yeye, ikiwa ni vitu vilivyo juu ya nchi, au vilivyo mbinguni.
Wakolosai 1:19-20 Biblia Habari Njema (BHN)
Maana Mungu alipenda utimilifu wake wote uwe ndani yake. Kwake vitu vyote vilipatanishwa na Mungu: Na kwa damu yake msalabani akafanya amani na vitu vyote duniani na mbinguni.
Wakolosai 1:19-20 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kwa kuwa katika yeye ilipendeza utimilifu wote ukae; na kwa yeye kuvipatanisha vitu vyote na nafsi yake akiisha kufanya amani kwa damu ya msalaba wake; kwa yeye, ikiwa ni vitu vilivyo juu ya nchi, au vilivyo mbinguni.
Wakolosai 1:19-20 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kwa kuwa katika yeye ilipendeza utimilifu wote ukae; na kwa yeye kuvipatanisha vitu vyote na nafsi yake akiisha kufanya amani kwa damu ya msalaba wake; kwa yeye, ikiwa ni vitu vilivyo juu ya nchi, au vilivyo mbinguni.
Wakolosai 1:19-20 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Kwa kuwa ilimpendeza Mungu kwamba utimilifu wake wote ukae ndani yake, na kupitia kwake aweze kuvipatanisha vitu vyote kwake mwenyewe, viwe ni vitu vilivyo duniani au vilivyo mbinguni, kwa kufanya amani kwa damu yake iliyomwagika msalabani.