Amosi 5:6-9
Amosi 5:6-9 Biblia Habari Njema (BHN)
Mtafuteni Mwenyezi-Mungu, nanyi mtaishi! La sivyo, atawalipukia wazawa wa Yosefu kama moto; moto utawateketeza wakazi wa Betheli na hakuna mtu atakayeweza kuuzima. Tahadhari enyi mnaogeuza haki kuwa uchungu, na kuuona uadilifu kuwa kama takataka! Huyo aliyezifanya Kilimia na sayari Orioni, ambaye huligeuza giza nene kuwa mchana, na mchana kuwa usiku; yeye ambaye ayaitaye pamoja maji ya bahari na kuyamwaga juu ya nchi kavu, Mwenyezi-Mungu ndilo jina lake. Yeye ndiye anayewaangamiza wenye nguvu, na kuziharibu ngome zao.
Amosi 5:6-9 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mtafuteni BWANA, nanyi mtaishi; asije akawaka kama moto katika nyumba ya Yusufu, nao ukateketeza, asiwepo mtu awezaye kuuzima katika Betheli. Ninyi mnaogeuza hukumu kuwa uchungu, na kuiangusha haki chini, mtafuteni yeye afanyaye Kilimia na Orioni, na kukigeuza kivuli cha mauti kuwa asubuhi, na kuufanya mchana kuwa giza usiku; yeye ayaitaye maji ya bahari, na kuyamwaga juu ya uso wa nchi; BWANA, ndilo jina lake; yeye aletaye uharibifu wa ghafla juu ya wenye nguvu, hata kuiharibu ngome.
Amosi 5:6-9 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mtafuteni BWANA, nanyi mtaishi; asije akawaka kama moto katika nyumba ya Yusufu, nao ukateketeza, asiwepo mtu awezaye kuuzima katika Betheli. Ninyi mnaogeuza hukumu kuwa uchungu, na kuiangusha haki chini, mtafuteni yeye afanyaye Kilimia na Orioni, na kukigeuza kivuli cha mauti kuwa asubuhi, na kuufanya mchana kuwa giza kwa usiku; yeye ayaitaye maji ya bahari, na kuyamwaga juu ya uso wa nchi; BWANA, ndilo jina lake; yeye aletaye uharibifu wa ghafula juu yao walio hodari, hata uharibifu uipate ngome.
Amosi 5:6-9 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Mtafuteni BWANA mpate kuishi, au atafagia nyumba ya Yusufu kama moto; utawateketeza, nayo Betheli haitakuwa na yeyote wa kuuzima. Ninyi ambao mnageuza haki kuwa uchungu na kuiangusha haki chini (yeye ambaye alifanya Kilimia na Orioni, ambaye hugeuza giza kuwa mapambazuko na mchana kuwa usiku, ambaye huyaita maji ya bahari na kuyamwaga juu ya nchi: BWANA ndilo jina lake; yeye hufanya maangamizi kwenye ngome na kufanya mji uliozungushiwa ngome kuwa ukiwa)