Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Amosi 5

5
Maombolezo kwa ajili ya dhambi ya Israeli
1 # Yer 7:29 Lisikieni neno hili nilitamkalo liwe maombolezo juu yenu, enyi nyumba ya Israeli.
2Bikira wa Israeli ameanguka;
hatainuka tena;
Ameangushwa katika nchi yake;
hakuna mtu wa kumwinua.
3Kwa kuwa Bwana MUNGU asema hivi; Mji uliotoka nje wenye watu elfu moja, utabakiziwa watu mia moja, na mji uliotoka wenye watu mia moja, utabakiziwa watu kumi, kwa nyumba ya Israeli. 4#2 Nya 15:2; Isa 55:3 Maana BWANA awaambia hivi nyumba ya Israeli, Nitafuteni mimi, nanyi mtaishi; 5#Amo 4:4; 8:14 bali msitafute Betheli, wala msiingie Gilgali, wala msipite kwenda Beer-sheba; kwani Gilgali hakika yake itakwenda utumwani, na Betheli itakuwa ubatili. 6Mtafuteni BWANA, nanyi mtaishi; asije akawaka kama moto katika nyumba ya Yusufu, nao ukateketeza, asiwepo mtu awezaye kuuzima katika Betheli. 7Ninyi mnaogeuza hukumu kuwa uchungu, na kuiangusha haki chini, 8#Ayu 9:9; 38:31,34; Amo 4:13 mtafuteni yeye afanyaye Kilimia na Orioni, na kukigeuza kivuli cha mauti kuwa asubuhi, na kuufanya mchana kuwa giza usiku; yeye ayaitaye maji ya bahari, na kuyamwaga juu ya uso wa nchi; BWANA, ndilo jina lake; 9yeye aletaye uharibifu wa ghafla juu ya wenye nguvu, hata kuiharibu ngome. 10#Isa 29:21; 1 Fal 22:8 Wao humchukia yeye akemeaye langoni, nao humzira anenaye maneno ya adili. 11#Mik 6:15; Sef 1:13 Basi, kwa kuwa mnamkanyaga maskini, na kumtoza ngano; ninyi mmejenga nyumba za mawe yaliyochongwa, lakini hamtakaa ndani yake; ninyi mmepanda mashamba mazuri ya mizabibu, lakini hamtakunywa divai yake. 12#Isa 29:21 Maana mimi najua jinsi maasi yenu yalivyo mengi, na jinsi dhambi zenu zilivyo kubwa; ninyi mnaowaonea wenye haki, mnaopokea rushwa, na kuwageuza wahitaji langoni wasipate haki yao. 13Kwa ajili ya hayo mwenye busara atanyamaza kimya wakati kama huo; kwa kuwa ni wakati mbaya. 14#Zab 34:12-16; Mit 11:27; Isa 1:16,17; Mik 6:8; Mt 7:7; Rum 2:7-9; Mik 3:11 Tafuteni mema, wala si mabaya, mpate kuishi; hivyo BWANA, Mungu wa majeshi, atakuwa pamoja nanyi, kama msemavyo. 15#Rum 12:9; Kut 32:30 Yachukieni mabaya; yapendeni mema; mkaithibitishe haki langoni; yamkini kwamba BWANA, Mungu wa majeshi, atawafanyia fadhili mabaki ya Yusufu. 16#Yer 9:17 Kwa ajili ya hayo, asema BWANA, Mungu wa majeshi, aliye Bwana; Kutakuwako maombolezo katika njia kuu zote; nao watasema katika njia zote, Ole! Ole! Nao watamwita mkulima aje kuombolea, na hao walio hodari wa kulia waje kuomboleza. 17#Kut 12:12 Tena katika mashamba yote ya mizabibu kutakuwako kulia; kwa maana mimi nitapita katikati yako, asema BWANA.
Siku ya BWANA; siku ya giza
18 # Isa 5:19; Eze 12:22; Mal 3:1; 2 Pet 3:4 Ole wenu! Ninyi mnaoitamani siku ya BWANA; kwa nini kuitamani siku ya BWANA? Ni giza, wala si nuru. 19Ni kama mtu aliyemkimbia simba, akakutana na dubu; au aliingia katika nyumba akauegemeza mkono wake ukutani, nyoka akamwuma. 20Je! Siku ya BWANA haitakuwa giza, wala si nuru? Naam, yenye giza sana, wala haina mwanga. 21#Isa 1:11 Mimi nazichukia sikukuu zenu, nazidharau, nami sitapendezwa na makutano yenu ya dini. 22Naam, ijapokuwa mnanitolea sadaka zenu za kuteketezwa na sadaka zenu za unga, sitazikubali; wala sitaziangalia sadaka zenu za amani, na za wanyama walionona. 23Niondoleeni kelele za nyimbo zenu; kwa maana sitaki kuzisikia sauti za vinanda vyenu. 24Lakini hukumu na iteremke kama maji, na haki kama maji makuu. 25#Mdo 7:42 Je! Mliniletea dhabihu na sadaka jangwani muda wa miaka arubaini, enyi nyumba ya Israeli? 26Naam, mtamchukua Sikuthi, mfalme wenu, na Kiuni, sanamu zenu, nyota ya mungu wenu, mliojifanyia wenyewe. 27Kwa sababu hiyo nitawapeleka uhamishoni, mwende mbali kupita Dameski, asema BWANA, ambaye jina lake ni Mungu wa majeshi.

Iliyochaguliwa sasa

Amosi 5: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha