Amosi 5:14-15
Amosi 5:14-15 Biblia Habari Njema (BHN)
Tafuteni kutenda mema na si mabaya, ili nyinyi mpate kuishi naye Mwenyezi-Mungu wa majeshi awe pamoja nanyi kama mnavyosema. Chukieni uovu, pendeni wema, na kudumisha haki mahakamani. Yamkini Mwenyezi-Mungu wa majeshi atawafadhili watu wa Yosefu waliobaki.
Amosi 5:14-15 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Tafuteni mema, wala si mabaya, mpate kuishi; hivyo BWANA, Mungu wa majeshi, atakuwa pamoja nanyi, kama msemavyo. Yachukieni mabaya; yapendeni mema; mkaithibitishe haki langoni; yamkini kwamba BWANA, Mungu wa majeshi, atawafanyia fadhili mabaki ya Yusufu.
Amosi 5:14-15 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Tafuteni mema, wala si mabaya, mpate kuishi; hivyo BWANA, Mungu wa majeshi, atakuwa pamoja nanyi, kama msemavyo. Yachukieni mabaya; yapendeni mema; mkaithibitishe haki langoni; yamkini kwamba BWANA, Mungu wa majeshi, atawafanyia fadhili mabaki ya Yusufu.
Amosi 5:14-15 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Tafuteni mema, wala si mabaya, ili mpate kuishi. Ndipo BWANA Mungu wa majeshi atakuwa pamoja nanyi, kama msemavyo yupo nanyi. Yachukieni maovu, yapendeni mema; dumisheni haki mahakamani. Yamkini BWANA Mungu wa majeshi atawahurumia mabaki ya Yusufu.