Amosi 3:4-8
Amosi 3:4-8 Biblia Habari Njema (BHN)
Je, simba hunguruma porini kama hajapata mawindo? Je, mwanasimba hunguruma pangoni mwake kama hajakamata kitu? Je, mtego bila chambo utamnasa ndege? Je, mtego hufyatuka bila kuguswa na kitu? Je, baragumu ya vita hulia mjini bila kutia watu hofu? Je, mji hupatwa na janga asilolileta Mungu? Hakika, Bwana Mwenyezi-Mungu hafanyi kitu bila kuwafunulia watumishi wake manabii nia yake. Simba akinguruma, ni nani asiyeogopa? Bwana Mwenyezi-Mungu akinena, ni nani atakataa kuutangaza ujumbe wake?
Amosi 3:4-8 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Je! Simba atanguruma mwituni, asipokuwa na mawindo? Mwanasimba atalia pangoni mwake, ikiwa hakupata kitu? Je! Ndege ataanguka mtegoni juu ya nchi, mahali asipotegewa tanzi? Mtego utafyatuka juu ya nchi, bila kunasa kitu chochote? Je! Tarumbeta itapigwa mjini, watu wasiogope? Mji utapatikana na hali mbaya, asiyoileta BWANA? Hakika Bwana MUNGU hatafanya neno lolote, bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake. Simba amekwisha kunguruma, ni nani asiyeogopa? Bwana MUNGU amenena, ni nani awezaye neno ila kutabiri?
Amosi 3:4-8 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Je! Simba atanguruma mwituni, asipokuwa na mawindo? Mwana-simba atalia pangoni mwake, ikiwa hakupata kitu? Je! Ndege ataanguka mtegoni juu ya nchi, mahali asipotegewa tanzi? Mtego utafyatuka juu ya nchi, bila kunasa kitu cho chote? Je! Tarumbeta itapigwa mjini, watu wasiogope? Mji utapatikana na hali mbaya, asiyoileta BWANA? Hakika Bwana MUNGU hatafanya neno lo lote, bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake. Simba amekwisha kunguruma, ni nani asiyeogopa? Bwana MUNGU amenena, ni nani awezaye neno ila kutabiri?
Amosi 3:4-8 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Je, simba hunguruma katika kichaka wakati hana mawindo? Aweza kuvuma katika pango wakati ambao hajakamata chochote? Je, ndege aweza kuanguka kwenye mtego ulio ardhini ambapo hajategewa chambo? Je, mtego unaweza kufyatuka toka ardhini wakati hakuna chochote cha kunasa? Je, tarumbeta inapopigwa mjini kujulisha hatari, watu hawatetemeki? Mji unapopatwa na maafa, je, si BWANA amesababisha? Hakika BWANA Mwenyezi hatafanya neno lolote bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake. Simba amenguruma: je, ni nani ambaye hataogopa? BWANA Mwenyezi ametamka: je, ni nani awezaye kukosa kutoa unabii?