Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Amosi 3:4-8

Amosi 3:4-8 BHN

Je, simba hunguruma porini kama hajapata mawindo? Je, mwanasimba hunguruma pangoni mwake kama hajakamata kitu? Je, mtego bila chambo utamnasa ndege? Je, mtego hufyatuka bila kuguswa na kitu? Je, baragumu ya vita hulia mjini bila kutia watu hofu? Je, mji hupatwa na janga asilolileta Mungu? Hakika, Bwana Mwenyezi-Mungu hafanyi kitu bila kuwafunulia watumishi wake manabii nia yake. Simba akinguruma, ni nani asiyeogopa? Bwana Mwenyezi-Mungu akinena, ni nani atakataa kuutangaza ujumbe wake?

Soma Amosi 3