2 Wathesalonike 2:10-12
2 Wathesalonike 2:10-12 Biblia Habari Njema (BHN)
na kutumia udanganyifu wa kila namna kwa wale walio katika mkumbo wa kupotea. Hao watapotea kwa sababu hawakuupokea na kuupenda ule ukweli ili waokolewe. Ndiyo maana Mungu amewaweka chini ya nguvu ya upotovu, wauamini uongo. Matokeo yake ni kwamba wote wasioamini ukweli, bali wanafurahia dhambi, watahukumiwa.
2 Wathesalonike 2:10-12 Swahili Revised Union Version (SRUV)
na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa. Kwa hiyo Mungu anawaletea upotevu mwingi, wauamini uongo; ili wahukumiwe wote ambao hawakuiamini kweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu.
2 Wathesalonike 2:10-12 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa. Kwa hiyo Mungu awaletea nguvu ya upotevu, wauamini uongo; ili wahukumiwe wote ambao hawakuiamini kweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu.
2 Wathesalonike 2:10-12 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
na katika njia zote ambazo uovu hudanganya wanaoangamia. Wanaangamia kwa sababu walikataa kuipenda kweli ili wapate kuokolewa. Kwa sababu hii, Mungu anawatumia nguvu ya udanganyifu, ili waamini uongo, na hivyo wahukumiwe wote ambao hawakuiamini ile kweli, bali wamefurahia uovu.