Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Wathesalonike 2

2
Mtu wa uvunjaji sheria
1 # 1 The 4:15-17 Basi, ndugu, tunawasihini, kuhusu kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo, na kukusanyika kwetu mbele zake, 2kwamba msifadhaishwe upesi hata kuiacha nia yenu, wala msishtushwe, kwa roho, wala kwa neno, wala kwa barua inayodhaniwa kuwa ni yetu, kana kwamba siku ya Bwana imekwisha kuwapo. 3#1 Tim 4:1; Yn 17:12; 1 Yoh 2:18; 4:3 Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yoyote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu; 4#Dan 11:36; Eze 28:2 yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama cha kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akijionesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu. 5Je! Hamkumbuki ya kuwa wakati nilipokuwapo pamoja nanyi niliwaambia hayo? 6Na sasa lizuialo mnalijua, yule apate kufunuliwa wakati wake. 7#Mdo 20:29 Maana ile siri ya kuasi hivi sasa inafanya kazi; lakini yuko azuiaye sasa, hadi atakapoondolewa. 8#Isa 11:4; Ayu 4:9; Ufu 19:15,20 Hapo ndipo atakapofunuliwa yule mwasi, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa dhihirisho la kuja kwake; 9#Mt 24:24; Ufu 13:11-13 kuja kwa yule mwasi ni kazi ya Shetani, atumiaye uwezo wote, ishara na ajabu za uongo; 10#2 Kor 2:15; 4:3 na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa. 11#2 Tim 4:4 Kwa hiyo Mungu anawaletea upotevu mwingi, wauamini uongo; 12ili wahukumiwe wote ambao hawakuiamini kweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu.
Waliochaguliwa kwa wokovu
13 # Efe 1:4; Kum 33:12; 1 The 2:13; 4:7 Lakini imetupasa sisi kumshukuru Mungu sikuzote kwa ajili yenu, ndugu mliopendwa na Bwana, kwa kuwa Mungu amewachagua tangu mwanzo mpate wokovu, katika kutakaswa na Roho, na kuiamini kweli; 14#1 The 4:7; 5:9 aliyowaitia ninyi kwa Injili yetu, ili kuupata utukufu wa Bwana wetu Yesu Kristo. 15Basi, ndugu, simameni imara, mkayashike mapokeo mliyofundishwa, ama kwa maneno, ama kwa barua yetu. 16#1 The 3:11-13 Na Bwana wetu Yesu Kristo mwenyewe, na Mungu Baba yetu, aliyetupenda akatupa faraja ya milele na tumaini jema, katika neema, 17awafariji mioyo yenu, na kuwafanya imara katika kila neno na tendo jema.

Iliyochaguliwa sasa

2 Wathesalonike 2: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha