1 Samueli 11:14-15
1 Samueli 11:14-15 Biblia Habari Njema (BHN)
Samueli akawaambia, “Twendeni wote Gilgali na kwa mara nyingine tutamtangaza Shauli kuwa mfalme.” Watu wote wakaenda Gilgali, na walipofika huko, wakamtawaza Shauli kuwa mfalme mbele ya Mwenyezi-Mungu. Wakamtolea Mwenyezi-Mungu tambiko za amani hapo. Na Shauli pamoja na watu wote wa Israeli wakafurahi sana.
1 Samueli 11:14-15 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kisha Samweli akawaambia watu, Haya! Na twendeni mpaka Gilgali, ili tuuanzishe ufalme upya huko. Nao watu wote wakaenda Gilgali; wakamtawaza Sauli mbele za BWANA huko Gilgali; wakachinja sadaka za amani mbele za BWANA; na huko Sauli na watu wote wa Israeli wakafurahi sana.
1 Samueli 11:14-15 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kisha Samweli akawaambia watu, Haya! Na twendeni mpaka Gilgali, ili tuuimarishe ufalme huko mara ya pili. Nao watu wote wakaenda Gilgali; wakamtawaza Sauli mbele za BWANA huko Gilgali; wakachinja sadaka za amani mbele za BWANA; na huko Sauli na watu wote wa Israeli wakafurahi sana.
1 Samueli 11:14-15 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Ndipo Samweli akawaambia watu, “Njooni, twendeni Gilgali na huko tuthibitishe ufalme.” Kwa hiyo watu wote wakaenda Gilgali na kumthibitisha Sauli kuwa mfalme mbele za BWANA. Huko wakatoa dhabihu za sadaka za amani mbele za BWANA, naye Sauli na Waisraeli wote wakafanya karamu kubwa.