1 Wakorintho 7:19-21
1 Wakorintho 7:19-21 Biblia Habari Njema (BHN)
Maana kutahiriwa au kutotahiriwa si kitu; kilicho muhimu ni kuzishika amri za Mungu. Basi, kila mmoja na abaki kama alivyokuwa wakati alipoitwa. Je, wewe ulikuwa mtumwa wakati ulipoitwa? Sawa, usijali; lakini ukipata fursa ya kuwa huru, itumie.
1 Wakorintho 7:19-21 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kutahiriwa si kitu, na kutotahiriwa si kitu bali kuzihifadhi amri za Mungu. Kila mtu na akae katika hali ile ile ambayo alikuwa nayo alipoitwa. Je! Uliitwa u mtumwa? Usione ni vibaya lakini kama ukiweza kuwa na uhuru, afadhali kuutumia.
1 Wakorintho 7:19-21 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kutahiriwa si kitu, na kutokutahiriwa si kitu bali kuzihifadhi amri za Mungu. Kila mtu na akae katika hali ile ile ambayo alikuwa nayo alipoitwa. Je! Uliitwa u mtumwa? Usione ni vibaya lakini kama ukiweza kuwa na uhuru, afadhali kuutumia.
1 Wakorintho 7:19-21 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Kutahiriwa si kitu, na kutokutahiriwa si kitu. Lakini kuzitii amri za Mungu ndilo jambo muhimu. Basi kila mmoja wenu na abaki katika hali aliyoitwa nayo. Je, wewe ulipoitwa ulikuwa mtumwa? Jambo hilo lisikusumbue. Ingawaje unaweza kupata uhuru, tumia nafasi uliyo nayo sasa kuliko wakati mwingine wowote.