1 Wakorintho 16:1-4
1 Wakorintho 16:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Sasa, yahusu ule mchango kwa ajili ya watu wa Mungu: Fanyeni kama nilivyoyaagiza makanisa ya Galatia. Kila Jumapili kila mmoja wenu atenge kiasi cha fedha kadiri ya mapato yake, ili kusiwe na haja ya kufanya mchango wakati nitakapokuja. Wakati nitakapokuja kwenu, nitawatuma wale mtakaowachagua miongoni mwenu wapeleke barua na zawadi zenu Yerusalemu. Kama itafaa nami niende, basi, watakwenda pamoja nami.
1 Wakorintho 16:1-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kuhusu ile michango kwa ajili ya watakatifu, kama vile nilivyoamuru makanisa ya Galatia, nanyi fanyeni vivyo hivyo. Siku ya kwanza ya juma kila mmoja wenu na aweke akiba kwake, kwa kadiri ya kufanikiwa kwake; ili kwamba michango isifanyike hapo nitakapokuja; nami nitakapofika nitawatuma kwa barua wale mtakaowachagua, wachukue hisani yenu mpaka Yerusalemu. Na kama ikifaa niende na mimi, watasafiri pamoja nami.
1 Wakorintho 16:1-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kwa habari ya ile changizo kwa ajili ya watakatifu, kama vile nilivyoamuru makanisa ya Galatia, nanyi fanyeni vivyo. Siku ya kwanza ya juma kila mtu kwenu na aweke akiba kwake, kwa kadiri ya kufanikiwa kwake; ili kwamba michango isifanyike hapo nitakapokuja; nami nitakapofika nitawatuma kwa nyaraka wale mtakaowachagua, wachukue hisani yenu mpaka Yerusalemu. Na kama ikifaa niende na mimi, watasafiri pamoja nami.
1 Wakorintho 16:1-4 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Basi kuhusu changizo kwa ajili ya watakatifu: Kama nilivyoyaagiza makanisa ya Galatia, fanyeni vivyo hivyo. Siku ya kwanza ya kila juma, kila mmoja wenu atenge kiasi cha fedha, kulingana na mapato yake, na fedha hizo aziweke akiba, ili nitakapokuja pasiwe na lazima ya kufanya mchango. Kwa hiyo nitakapowasili, nitawapa wale mtakaowachagua barua za kuwatambulisha, ili kuwatuma wapeleke zawadi zenu huko Yerusalemu. Ikionekana ni vyema na mimi niende, basi hao watu watafuatana nami.