Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Kor 16

16
Michango kwa Watakatifu
1 # Rum 15:25-26; Mdo 11:29; Gal 2:10; 2 Kor 8:9 Kwa habari ya ile changizo kwa ajili ya watakatifu, kama vile nilivyoamuru makanisa ya Galatia, nanyi fanyeni vivyo. 2#Mdo 20:7Siku ya kwanza ya juma kila mtu kwenu na aweke akiba kwake, kwa kadiri ya kufanikiwa kwake; ili kwamba michango isifanyike hapo nitakapokuja; 3nami nitakapofika nitawatuma kwa nyaraka wale mtakaowachagua, wachukue hisani yenu mpaka Yerusalemu. 4Na kama ikifaa niende na mimi, watasafiri pamoja nami.
Mipango ya Usafiri
5 # Mdo 19:21 Lakini nitakuja kwenu, nikiisha kupita kati ya Makedonia; maana napita kati ya Makedonia. 6#Rum 15:24; Tit 3:12Labda nitakaa kwenu; naam, labda wakati wote wa baridi, mpate kunisafirisha ko kote nitakakokwenda. 7#Mdo 20:2; 18:21Maana sipendi kuonana nanyi sasa, katika kupita tu, kwa sababu nataraji kukaa kwenu muda kidogo, Bwana akinijalia. 8#Law 23:15-21; Kum 16:9-11; Mdo 19:1,10#Mdo 19:8-10Lakini nitakaa Efeso hata Pentekoste; 9#2 Kor 2:12; Kol 4:3; Ufu 3:8kwa maana nimefunguliwa mlango mkubwa wa kufaa sana, na wako wengi wanipingao.
10 # 1 Kor 4:17; Flp 2:20 Lakini, Timotheo akija, angalieni akae kwenu pasipo hofu; maana anaifanya kazi ya Bwana vile vile kama mimi mwenyewe; 11#1 Tim 4:12basi mtu ye yote asimdharau, lakini msafirisheni kwa amani, ili aje kwangu; maana ninamtazamia pamoja na ndugu zetu. 12#1 Kor 1:12; 3:6Lakini kwa habari za Apolo, ndugu yetu, nalimsihi sana aende kwenu pamoja na hao ndugu; ambaye si mapenzi yake kwenda sasa; lakini atakuja atakapopata nafasi.
Wasia wa Mwisho na Salamu
13 # Zab 31:24; Efe 6:10 Kesheni, simameni imara katika Imani, fanyeni kiume, mkawe hodari. 14Mambo yenu yote na yatendeke katika upendo.
15 # 1 Kor 1:16; Rum 16:5 Tena ndugu, nawasihi; (mnawajua watu wa nyumbani mwa Stefana kwamba ni malimbuko ya Akaya, nao wamejitia katika kazi ya kuwahudumu watakatifu); 16#Flp 2:29watiini watu kama hawa, na kila mtu afanyaye kazi pamoja nao, na kujitaabisha. 17Nami nafurahi kwa sababu ya kuja kwao Stefana na Fortunato na Akaiko; maana hawa wamenikirimia kwa wingi yale niliyopungukiwa kwenu. 18#1 The 5:12Maana wameniburudisha roho yangu, na roho zenu pia; basi wajueni sana watu kama hao.
19 # Mdo 18:2,18,26; Rum 16:3,5 Makanisa ya Asia wawasalimu. Akila na Priska wawasalimu sana katika Bwana, pamoja na kanisa lililoko ndani ya nyumba yao. 20#Rum 16:16; 2 Kor 13:12; 1 Pet 5:14Ndugu wote wawasalimu. Salimianeni kwa busu takatifu.
21 # Kol 4:18; 2 The 3:17 Hii ni salamu yangu Paulo kwa mkono wangu mwenyewe. 22#Gal 1:8,9Mtu awaye yote asiyempenda Bwana, na awe amelaaniwa. Maran atha.#16:22Maran atha maana yake ni, Bwana wetu anakuja. 23Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi. 24Pendo langu na liwe pamoja nanyi nyote katika Kristo Yesu.

Iliyochaguliwa sasa

1 Kor 16: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha