Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ufunuo 15

15
Misiba mikuu ya mwisho
1Kisha nikaona ishara nyingine mbinguni, kubwa na ya kushangaza. Palikuwa hapo malaika saba wenye mabaa saba ya mwisho. Kwa mabaa hayo saba, ghadhabu ya Mungu imekamilishwa.
2Kisha nikaona kitu kama bahari ya kioo, imechanganywa na moto. Nikawaona pia wale watu waliomshinda yule mnyama na sanamu yake na ambaye jina lake lilitajwa kwa ile tarakimu. Watu hao walikuwa wamesimama kando ya hiyo bahari ya kioo, wakiwa na vinubi walivyopewa na Mungu. 3Walikuwa wakiimba wimbo wa Mose, mtumishi wa Mungu na wa Mwanakondoo:
“Bwana Mungu Mwenye Nguvu,
matendo yako ni makuu na ya ajabu mno!
Ewe Mfalme wa mataifa,
njia zako ni za haki na za kweli!
4 # Taz Zab 86:9 Bwana, ni nani asiyekucha wewe?
Nani asiyelitukuza jina lako?
Wewe peke yako ni Mtakatifu.
Mataifa yote yatakujia na kukuabudu
maana matendo yako ya haki yamedhihirishwa.”
5Baada ya hayo nikaona hekalu limefunguliwa mbinguni, na ndani yake hema ya kuwapo kwa Mungu. 6Basi, wale malaika saba wenye mabaa saba wakatoka humo hekaluni, wakiwa wamevaa nguo za kitani safi zenye kung'aa na kanda za dhahabu vifuani mwao. 7Kisha, mmojawapo wa wale viumbe wanne akawapa hao malaika saba mabakuli ya dhahabu yaliyojaa ghadhabu ya Mungu, aishiye milele na milele. 8Hekalu likajaa moshi uliosababishwa na utukufu na nguvu ya Mungu, na hakuna mtu aliyeweza kuingia hekaluni mpaka mwisho wa mabaa saba ya wale malaika saba.

Iliyochaguliwa sasa

Ufunuo 15: BHN

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha