Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 62

62
Mungu mlinzi wangu
(Kwa Mwimbishaji: Mtindo wa Yeduthuni. Zaburi ya Daudi)
1Namngojea Mungu peke yake kwa utulivu,
kwake watoka wokovu wangu.
2Yeye peke yake ndiye mwamba na wokovu wangu,
yeye ni ngome yangu, sitatikisika.
3Hata lini mtanishambulia mimi?
Hata lini nyinyi nyote mtanipiga,
mimi niliye kama kiambaza kilichoinama,
kama ukuta unaoanza kubomoka?
4Mmepanga kuniangusha toka mahali pangu pa heshima;
furaha yenu ni kusema uongo.
Kwa maneno, mnabariki,
lakini moyoni mnalaani.
5Namngojea Mungu peke yake kwa utulivu;
kwake naliweka tumaini langu.
6Yeye peke yake ndiye mwamba na wokovu wangu,
yeye ni ngome yangu, sitatikisika.
7Wokovu na fahari yangu vyatoka kwa Mungu;
mwamba wangu mkuu na kimbilio langu ni Mungu.
8Enyi watu, mtumainieni Mungu daima;
mfungulieni Bwana yaliyo moyoni mwenu.
Mungu ndiye kimbilio la usalama wetu.
9Binadamu wote ni kama pumzi tu;
wote, wakubwa kwa wadogo, hawafai kitu.
Tena ukiwapima uzito hawafikii kilo,
wote pamoja ni wepesi kuliko pumzi.
10Msitegemee dhuluma,
msijisifie mali ya wizi;
kama mali zikiongezeka, msizitegemee.
11Mungu ametamka mara moja,
nami nimesikia tena na tena:
Kwamba enzi ni mali yake Mungu;
12 # Taz Mat 16:27; Rom 2:6; Ufu 2:23 naam, nazo fadhili ni zake Bwana;
humlipa kila mtu kadiri ya matendo yake.

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 62: BHN

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha