Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Methali 24:5-14

Methali 24:5-14 BHN

Kuwa na hekima ni bora kuliko kuwa na nguvu, naam, maarifa ni bora kuliko nguvu. Maana kwa mwongozo mzuri waweza kupigana vita, na kwa washauri wengi ushindi hupatikana. Kwa mpumbavu hekima ni ngumu kuielewa; penye mkutano wa mashauri hafungui mdomo. Afikiriaye kutenda maovu daima ataitwa mtu mwenye fitina. Mpango anaofikiria mpumbavu ni dhambi; mwenye dharau huchukiwa na kila mtu. Ukifa moyo wakati wa shida, basi wewe ni dhaifu kweli. Mwokoe mtu anayechukuliwa kuuawa bure; usisite kumwokoa anayeuawa bila hatia. Usiseme baadaye: “Hatukujua!” Maana Mungu apimaye mioyo ya watu huona; yeye atakulipa kulingana na matendo yako! Mwanangu, ule asali maana ni nzuri; sega la asali ni tamu mdomoni. Ndivyo ilivyo hekima nafsini mwako; ukiipata utakuwa na matazamio mema, wala tumaini lako halitakuwa la bure.

Soma Methali 24