Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yoshua 7:10-12

Yoshua 7:10-12 BHN

Mwenyezi-Mungu akamwambia Yoshua, “Simama! Mbona umejitupa chini hivyo? Waisraeli wametenda dhambi, maana wamelivunja agano langu nililowaamuru washike; wamevichukua baadhi ya vitu vilivyowekwa wakfu viangamizwe; wameviiba na kudanganya, wakaviweka pamoja na vitu vyao. Kwa hiyo Waisraeli hawawezi kuwakabili maadui zao; wanawakimbia adui zao kwa sababu wamejifanya wenyewe kuwa kitu cha kuangamizwa! Sitakuwa pamoja nao tena msipoharibu vitu vilivyomo kati yenu vilivyotolewa viangamizwe.

Soma Yoshua 7