Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yona 4:1-5

Yona 4:1-5 BHN

Lakini jambo hilo halikumpendeza Yona hata kidogo, akakasirika sana. Kwa hiyo akaomba, “Mwenyezi-Mungu, je, hayo si mambo yaleyale niliyowaza utayafanya nilipokuwa nyumbani? Ndio maana nilifanya haraka kukimbilia Tarshishi. Nilijua kwamba wewe u Mungu wa upendo na huruma. Hukasiriki upesi, daima u mwema na u tayari kubadili nia yako wakati wowote ili usiadhibu. Basi, sasa ee Mwenyezi-Mungu, nakusihi uniondolee uhai wangu, maana, kwangu mimi ni afadhali kufa kuliko kuishi.” Naye Mwenyezi-Mungu akamjibu Yona: “Unadhani wafanya vema kukasirika?” Ndipo Yona akatoka nje ya mji, akajikalia upande wa mashariki wa mji huo. Hapo, akajijengea kibanda, akaketi kivulini mwake huku anangojea apate kuona litakaloupata mji wa Ninewi.

Soma Yona 4