Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Waamuzi 14:1-3

Waamuzi 14:1-3 BHN

Siku moja, Samsoni aliteremka na kwenda Timna ambako alimwona msichana mmoja Mfilisti. Aliporudi nyumbani akawaambia wazazi wake, “Nimemwona msichana mmoja Mfilisti huko Timna. Niozeni msichana huyo.” Lakini wazazi wake wakamwambia, “Je, hakuna msichana yeyote miongoni mwa ndugu zako au kati ya watu wetu hata uende kuoa kwa Wafilisti wasiotahiriwa?” Lakini Samsoni akamwambia baba yake, “Niozeni msichana huyo, maana ananipendeza sana.”

Soma Waamuzi 14