Isaya 66:23-24 BHN
Katika kila sikukuu ya mwezi mpya,
na katika kila siku ya Sabato,
binadamu wote watakuja kuniabudu.
Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
“Kisha watakwenda kuziona maiti za wale walioniasi. Wadudu watakaowala hawatakufa, na moto utakaowachoma hautazimika kamwe. Watakuwa chukizo kwa watu wote.”