Nembo ya Programu ya Biblia
Ikoni ya Utafutaji

Isaya 66:23-24 - Linganisha Matoleo Yote

Isaya 66:23-24 BHN (Biblia Habari Njema)

Katika kila sikukuu ya mwezi mpya, na katika kila siku ya Sabato, binadamu wote watakuja kuniabudu. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema. “Kisha watakwenda kuziona maiti za wale walioniasi. Wadudu watakaowala hawatakufa, na moto utakaowachoma hautazimika kamwe. Watakuwa chukizo kwa watu wote.”

Shirikisha
Isaya 66 BHN

Isaya 66:23-24 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)

Na itakuwa, mwezi mpya hata mwezi mpya, na sabato hata sabato, wanadamu wote watakuja kuabudu mbele zangu, asema BWANA. Nao watatoka nje na kuitazama mizoga ya watu walioniasi; maana funza wao hatakufa, wala moto wao hautazimika nao watakuwa chukizo machoni pa wote wenye mwili.

Shirikisha
Isaya 66 SUV

Isaya 66:23-24 SRUV (Swahili Revised Union Version)

Na itakuwa, mwezi mpya hata mwezi mpya, na sabato hata sabato, wanadamu wote watakuja kuabudu mbele zangu, asema BWANA. Nao watatoka nje na kuitazama mizoga ya watu walioniasi; maana funza wao hatakufa, wala moto wao hautazimika nao watakuwa chukizo machoni pa wote wenye mwili.

Shirikisha
Isaya 66 SRUV

Isaya 66:23-24 NEN (Neno)

Kutoka Mwezi Mpya hata mwingine, na kutoka Sabato hadi nyingine, wanadamu wote watakuja na kusujudu mbele zangu,” asema BWANA. “Nao watatoka nje na kuona maiti za wale walioniasi mimi. Funza wao hawatakufa, wala moto wao hautazimika, nao watakuwa kitu cha kuchukiza sana kwa wanadamu wote.”

Shirikisha
Isaya 66 NEN